Serikali yazidiwa nguvu kodi ya simu

Serikali yazidiwa nguvu kodi ya simu

bulama

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
561
Reaction score
135
Dar es Salaam. Kuna kila dalili kwamba Serikali inajipanga kufuta kodi ya Sh1,000 kila mwezi kwa wamiliki wa laini za simu baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, taasisi na baadhi ya kampuni za simu nchini.

Hiyo inatokana na kauli ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba aliyoitoa jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya Makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, CCM, kukaririwa na vyombo vya habari kikiitaka Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato badala ya tozo hiyo.

Akizungumza kwa simu jana Makamba alisema: "Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi."

Alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano zinapungua... "Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.

"Nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo."

Jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema kwamba Serikali inapokea maoni ya wadau mbalimbali ili kuona namna ya kufanya marekebisho ya tozo hiyo. Hata hivyo, alisema uamuzi wa kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa Serikali bali ulipitishwa na kukubaliwa baada ya kujadiliana na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.

"Hayo yalipendekezwa na Kamati ya Bunge siyo Serikali. Tena walipendekeza vyanzo 67 vya kodi likiwamo hilo la kadi za simu. Walipendekeza tukate Sh1,450 kwa mwezi, lakini sisi Serikali tukashusha hadi Sh1,000 yaani kila mwananchi akatwe Sh33.3 kwa siku na mapato yatakayopatikana yatakwenda kuboresha miradi ya maji, umeme vijijini na barabara," alisema Dk Mgimwa.

Upinzani mkali

Wabunge wa Chadema, John Mnyika wa (Ubungo) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), wamekuwa mstari wa mbele kupinga kodi kwa kuonyesha jinsi itakavyowanyanyasa wananchi.

Mnyika amekuwa akikusanya saini za wananchi wanaopinga mpango huo wa Serikali ili awasilishe bungeni hoja ya wananchi kupinga tozo hiyo. Hadi sasa ameshakusanya saini zaidi ya 26,000.

Kwa upande wake, Zitto alisema kodi hiyo haikujadiliwa kabisa kwa kuwa iliondolewa katika mapendekezo ya mapato lakini ikarejeshwa kupitia Muswada wa Fedha ambao hutafsiri hotuba ya Bajeti kisheria.

"Kama kodi hii haikuwa kwenye hutuba, haikujadiliwa na Bunge, msingi wa Muswada wa Fedha kuwa na kodi hii haupo. Kodi hii ilirejeshwa kinyemela bungeni na kupitishwa bila mjadala.

Chanzo:
Mwananchi
 
siyo kujichanganya serikali ya ccm ni serikali sikivu.
 
Hakuna usikiv uwowotw hapa..sema serikali ya CCM ni kurupukaji.
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
 
Kama Naibu waziri wa Mawasiliano anapingana na Waziri wa fedha hadharani juu ya kitu ambacho wao wamekipitisha hii ina maana gani zaidi ya kukurupuka??

Kwa nini wasiwe na kauli moja ambayo tutaiita kauli ya serikali???
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
kodi ilipitishwa na wabunge wote wa ccm kwa kusema ndiooooooooooooooooooo.sasa wewe unasema ccm inapinga!au unaongea kama kiongozi wa CCJ?
 
Hata sishangazwi na mkanganyiko wa kauli za viongozi hawa wa serikali ya ccm maana kila mtu ndani ya serikali na chama ni msemaj!shem on them
 
Dah! Hata mm nashangaa hawa wanaosema serikali ilipinga kodi hiyo. Kama ndiyo ililetwa na nani? Na aliyefikisha hapa tulipo ni nani? Tuache fikra dumavu katika masuala ya msingi kwa wananchi.
 
Sijawahi kuona Serikali ya ajabu kama hii jamani!Wanatuongezea kodi wakidai hawana fedha za kutosha kukamilisha baadhi ya miradi ya maendeleo hapo hapo zinakuja taarifa kuwa kuna ufisadi wa mabilioni ya shilingi umefanyika siku ya ziara ya Obama wakati wa mkutano wa Smart Partnership sasa kumbe haya ndio maeneo muhimu Serikali inapaswa kuyaangalia na kupapambana nayo ili kuokoa mabilioni ya shilingi yanayopotea kila siku.

Pia Serikali ipunguze matumizi makubwa yasio ya lazima ili pia kuyaokoa mabilioni ya shilingi yanayopotelea katika miradi au shughuli zisizokuwa na manufaa yoyote kwa Wananchi.Serikali wakifanya haya hakutakuwa tena na haja ya kumlundikia Mtanzania mzigo wa kodi kama vile kodi za mishahara (PAYE), Kodi za Simcard, Kodi za leseni ya biashara na tozo nyinginezo ambazo zimejaa usumbufu mkubwa kwa Wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Pia hata baadhi ya VAT zingeondoka katika bidhaa na huduma kwasababu tu Serikali tu Serikali inayo fedha ya kutosha hazina kuendesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
 
siyo kujichanganya serikali ya ccm ni serikali sikivu.

Bunge la ndioooooo! hata pale pasipo na maslahi kwa Watanzania wao ni ndiooooo, na matusi na kejeli kwamba wao wako wengi bungeni. Mimi nashauri Watanzania nasi tuseme siyooooo kwa wabunge wa ccm ambao hawatujali
 
Hapo ndo mjiulize maswali wale mlioipigia kura CCM na wabunge wake, waokila kitu ni ndioooooooooo
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
Mnatafuta Hela za kampeni wakati mnajua mpo ICU? Sasa hela za madini mnapeleka wapi au kwenye hiyo mitumbo yenu mikubwa kama mithili ya wale wa mama waliotimiza miezi tisa ya ile kitu
 
siyo kujichanganya serikali ya ccm ni serikali sikivu.

Ila sijui ni kwa nini walipitisha Kodi ambayo walijua kabisa itawaumiza wananchi...
Inawezekana kweli ni Serikali Sikivu ila ni Serikali Kipofu, haioni, haitafakari mpaka watu wapige kelele....
 
SERIKALI INATAKA POLISI WAPIGE RAIA HATA KUUA, WABUNGE WANAO UNGA MKONO WASEME NDIYO NA WASIOAFIKI WASEME SIYO. NDIYOOOO! SIYOOOOOOOOOOOOOOOOO. WANAOAFIKI WAMESHINDA..tehe tehe!
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Hivi ninyi wanasiasa mbona mnafanya maamuzi bila kufanya/kutumia utafiti?

Matamko yenu siku zote yamekuwa yakiwagawa wananchi ina maana hamuwatumii

wataalamu kwa ushauri?

Sawa kwa sasa mnashinikiza kodi kuondolewa kwa hiyo hivyo vyanzo vingine mmekwisha vifanyia utafiti

kubaini kama navyo havitakuwa kikwazo kwa wananchi?

Vitu vingine sio kutangaza tangaza tu kwenye media mnahitajika kuchukua hatua zenye manufaa na sio

kuuma-uma maneno kwakua kufanya hivyo mtaonekana kana kwamba mnafanya dili zenu na si kwa

manufaa ya watu.

Siku zote mjitahidi kuwa na lugha ya pamoja katika kuwakilisha kitu/vitu vyenye maslahi ya wengi

vinginevyo mtaonekana kana kwamba mmekurupuka au mnatengenezo vitu vyenye majibu mepesi au
visivyowezekana ili mvitumie kujiimalisha kisiasa.

Binafsi napendekeza lipa kadri unavyotumia kama njia mojawapo ya kutunisha mfuko unaohitajika,

au ninyi wenyewe kwa kushirikiana na wenzenu mkatwe sehemu ya marupurupu yenu kutunisha mfuko huo.
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Mi nasema wapigwe tu! Maana tumeshachoka hata kufikiri kabla ya kuchukua hatua hatuwezi. Wakikataa kulipa hiyo kodi wapigwe tu.
 
Hiyo itakuwa kitu kingine make wateja mitandao ndo watakuwa wanalipa kodi ya mitandao badala ya kampuni lenyewe...
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Mkuu Nape Nnauye

Kwanza nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuchangia hapa JF kila unapoona jambo linakugusa kwa namna moja.

Hii Kodi ya Simu kwa ujumla ilipitishwa na Wabunge, na siku ya kuhitimisha Bajeti mle ndani ya Bunge kulikuwa na idadi kubwa sana ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wakiongozwa na mh. Spika. Hivyo sisi wananchi wa Tanzania tunasema kuwa ndio walioileta hii Kodi ambayo leo kila kona inalalamikiwa.

Walikosa busara katka kufikiria madhara ya jambo hili nao kwa upeo wao mdogo waliweka masilahi ya chama mbele kuliko ya wananchi (Walijisahau kuwa wanawakilisha wananchi na kwamba hawawakilishi Serikali pale Bungeni)

Ndugu yetu Napee katika kuliweka jambo hili sawa na mengineyenye mtizamo kama huu, ni wakati sasa wewe kwa nafasi yako katika Chama kuwaeleza Wabunge na wanachama kwa ujumla, kuwa kule Bungeni tutenganishe kati ya Mambo ya Chama na Serikali.

Bunge ni chombo cha Serikali na siyo chombo cha chama. Ndio maana hata bajeti inayotumika Bungeni siyo ya Chama bali ya Serikali.

Mbunge aingie Bungeni kama mwakilishi wa wananchi na siyo mwakilishi wa Chama.

Vinginevyo kusipokuwa na mabadiriko kuna hatari ya nchi kurudi nyuma kiuchumi kutokana na kila siku watu wanarumbana badala ya kujadili mambo ya maendeleo.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!
 
Last edited by a moderator:
Siamini macho na masikio yangu kua serikali imeshindwa kutafuta vyanzo vingine vya kodi kama kupitia vitu kama Alamasi/Tanzanite/Ureniam/Gas/Makaa ya mawe na vinginevyo vingi tu! Sasa ndio tuseme serikali haioni hivi mapaka kufikia kuweka kodi kwenye line za simu??? Hivi ni nani anayeishauri hii serikali ya CCM?
 
wabunge walipitisha,na inabidi wakae tena vikao ili kubatilisha! posho wasilipwe tena kwa upuuz wao wakutokuwa makini. nashauri wakae kikao wabadilishe hiyo sim card tax na posho watumie mishahara yao ili cku nyngne wawe makini!
 
Back
Top Bottom