Kaka
bulama hebu acha kueneza hizi propaganda za rejareja. Wanaotoa matamshi wote wanakinzana. Nilishaacha kuwaamini nduli hawa miaka kadhaa, hata kabla ya CHADEMA kupata umaarufu.
Najua wapo wengi ambao wamejitwisha kazi niliyoianzisha ya kususia MITANDAO YOTE ya simu, kwa siku moja, kazi niliyoiasisi. Serikali inaogopa kupoteza mapato ndio maana inakuja na danganya toto za ki-hunihuni tu, ili tuamini tumeishinda. Hizo ni propaganda ambazo watu kama wewe wamelipwa kuzieneza. Kaka au dada, kaa uelewe kwamba Watanzania wa leo si wale wa 2005, na hakika, Watanzania wa leo hawatafanana hata kidogo na wale wa 2015. Nini kimebadilika au kitabadilika? Soma alama za nyakati!
Nakutuma uende kwa hao waliokutuma ukawaambie kwamba mgomo wetu wa kuzima simu nchi nzima kwa mitandao yote, 19-08-13 hadi 20-08-13 kwa muda wa saa 24, yaani kuanzia saa 6 usiku hadi saa 6 usiku wa kesho yake, UKO PALE PALE.
Niko radhi kutokuwa na mawasiliano kwa siku moja, lakini siko tayari kuiunga mkono serikali iliyoasi wananchi wake na kuwageuza chanzo cha mapato haramu. Wizi wa mchana na ufisadi huu tunaupinga kwa nguvu zetu zote.
Wakiuliza nani kakutuma, waambie ni mimi Mwana wa Haki, a.k.a. MwanaHaki, Mzalendo Namba 1.
Siogopi kufa. Nikifa nitakufa kifo cha kishujaa, Mungu atanipokea mbibguni kwa kuwatetea watoto wake Watanzania, na atanilipia kisasi.
Isitoshe, nikifa mtakuwa mmechochea moto wa mashujaa wengine kuja nyuma yangu kwa mamia ya maelfu, kama si mamilioni.
Kazi ni kwenu!