Serikali yetu haioni ni hekima kuwatumia wafungwa kama vibarua wa Wakandarasi katika kuwapunguzia mzigo?

Serikali yetu haioni ni hekima kuwatumia wafungwa kama vibarua wa Wakandarasi katika kuwapunguzia mzigo?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Katika kandarasi nyingi wafanyakazi wasio rasmi /temporary worker aka vibarua, huigarimu kampuni almost 7-10, ya fedha za mradi although bajeti hii huwa imeainishwa ndani ya mkataba, tunashuhudia mataifa kama China hufanya haya, huwa kama ni sehemu ya wafungwa katika kufundishwa kazi mbalimbali za kijamii, kwa kulitumikia taifa lao kwa namna fulani,pia itaokoa gharama kwa kiasi fulani.

#ALAMSIKI
 
Na hiyo ndio maana halisi ya Mfungwa pale ni chuo wenye ujuzi wanawapa wasio na ujuzi kushirikiana na Serikali alafu unawatupa kwenye miradi mbalimbali ya kijamii,,lakini kwetu huku ni kulima mashamba ya viongozi
 
Wafungwa ni faida kubwa sana kwa nchi endapo watatumika vizuri, mataifa kama China huwa na mashamba ya Kitaifa, (National farms) ambayo Uhudumiwa na wafungwa, ni mbaya Sana kumtumia mfungwa katika kulima mashamba ya viongozi, wafungwa wakitumika vizuri ipo siku Jeshi la magereza litakuja kutoa gawio serekalini.
 
Wafanye kazi ambazo hata Kama wangekuwa nje wangefanya na sio kupasua kuni na Kubebeshwa zege

Au kulimishwa mashamba

Wafanye Kazi zenye utu zaidi
 
Unataka mashamba ya askali magereza yalimwe n nan?
Ni kweli wanayo mashamba lakini yanatumika katika very low au hayatumiki kikamilifu nendeni mkayaone!
Ilipaswa reserve ya NFRA, by 50% ya chakula cha reserve ijazwe na chakula toka mashamba ya kimkakati yanayosimamiwa na magereza kwa kutumia wafungwa.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Wafanye kazi ambazo hata Kama wangekuwa nje wangefanya na sio kupasua kuni na Kubebeshwa zege

Au kulimishwa mashamba

Wafanye Kazi zenye utu zaidi
Wakikodiwa na Wakandarasi wakubwa fedha zitaingia serekalini /magereza, wakilima vyema kwa 100%,nao pia watapata chakula bora zaidi, ikibidi milo mitatu, sio utu, kwa sababu ni mfungwa akala mlo mmoja kwa kutwa wenye mashaka!, wawe kikazi zaidi na sio kuwa mzigo kwa serekali.
 
Hao wafungwa kila siku jioni atakuwa anapungua mmoja,kutokana na mfumo wetu wa ulinzi ulivyo
 
Katika kandarasi nyingi wafanyakazi wasio rasmi /temporary worker aka vibarua, huigarimu kampuni almost 7-10, ya fedha za mradi although bajeti hii huwa imeainishwa ndani ya mkataba, tunashuhudia mataifa kama China hufanya haya, huwa kama ni sehemu ya wafungwa katika kufundishwa kazi mbalimbali za kijamii, kwa kulitumikia taifa lao kwa namna fulani,pia itaokoa gharama kwa kiasi fulani.

#ALAMSIKI
Niwazo zuri Sana na itasaidia wafungwa kuludi uraiani na ujuzi utakao wafaa kwa maisha yao mapya
 
Ulidanganywa, China haiwatumii bure huwalipa fedha kama vibarua wengine, sema toa wazo wafungwa hasa wale wa muda mrefu washiriki miradi, na wale wanaokaribia kumaliza vifungo washiriki kwenye hiyo miradi ili wapate kipato na wapate pa kuanzia wakirudi uraiani, hiyo iitwe ( life skills) Kwa wafungwa
 
Back
Top Bottom