Serikali yetu imejiandaaje kukabiliana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola?

Serikali yetu imejiandaaje kukabiliana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
20,118
Reaction score
40,850
Habari wakuu!!

Kila mtu mwenye mazoea ya kupata habari ni shahidi wa yale yanayoendelea Nchini Congo juu ya mlipuko wa ugonjwa hatari wa EBOLA.

Kwa ujirani na maungiliano ya kibiashara baina yetu na Congo bila hata Sisi tupo kwenye hatari kubwa kuingiliwa na ugonjwa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa katika kuzuia hilo.

Je serikali yetu imechukua hatua gani za makusudi na za haraka katika kukabiliana na hilo janga hapa Nchini......!?
 
Habari wakuu!!

Kila mtu mwenye mazoea ya kupata habari ni shahidi wa yale yanayoendelea Nchini Congo juu ya mlipuko wa ugonjwa hatari wa EBOLA.

Kwa ujirani na maungiliano ya kibiashara baina yetu na Congo bila hata Sisi tupo kwenye hatari kubwa kuingiliwa na ugonjwa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa katika kuzuia hilo.

Je serikali yetu imechukua hatua gani za makusudi na za haraka katika kukabiliana na hilo janga hapa Nchini......!?
Gentleman,
serikali sikivu ya ccma tayari ilishatoa taarifa na hatua za awali ilizochukua kuhusu ugonjwa huo hatari wa maambukizi.


hebu tupate maelezo zaidi hapo chini,

Na Atley Kuni, WAF-Dodoma,
May 19th, 2026


Serikali kupitia Wizara ya Afya imewahakikishia wananchi kuwa hadi sasa Tanzania haina kisa chochote cha ugonjwa wa Ebola, huku ikiendelea kuimarisha hatua za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo baada ya nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda kuripoti mlipuko wa Ebola.

Akitoa taarifa kwa umma mjini Dodoma Mei 18, 2026, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuzuia ugonjwa huo kuingia nchini kutokana na mwingiliano mkubwa wa kijamii na kiuchumi uliopo kati ya Tanzania na nchi zilizoathirika.

Dkt. Magembe amesema Ebola husababishwa na virusi vinavyoenea kutoka kwa popo na wanyama jamii ya sokwe kwenda kwa binadamu, na baadaye kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia majimaji ya mwili wa mgonjwa au mtu aliyefariki kwa ugonjwa huo.

Amesema dalili za Ebola ni pamoja na homa, uchovu wa mwili, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa, kutapika na kuharisha. Baadhi ya wagonjwa wanaweza kupata vipele pamoja na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili kama macho, pua, masikio na mdomo.

"Serikali imeendelea kuimarisha uchunguzi wa afya kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia mipaka, bandari na viwanja vya ndege ili kubaini mapema viashiria vya ugonjwa huo" amesema Dkt. Magembe na kuongeza

"Serikali pia imepeleka wataalam katika mikoa yenye hatari kubwa na kuhakikisha vituo vya afya vina dawa, vifaa kinga na huduma muhimu za kukabiliana na Ebola endapo ugonjwa utaingia nchini" amesisitiza Dkt. Magembe

Wizara ya Afya imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia televisheni, redio na mitandao ya kijamii kuhusu njia za kujikinga na ugonjwa huo. Serikali pia imeimarisha ushirikiano na nchi jirani pamoja na kuhuisha mwongozo wa wasafiri kuanzia Mei 19, 2026 kwa mujibu wa Kanuni za Afya za Kimataifa.

Dkt. Magembe amewataka wananchi kuendelea kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kuepuka kugusa majimaji ya mwili ya mtu mwenye dalili za Ebola, na kuwahi hospitali endapo watapata dalili zinazofanana na ugonjwa huo.

Mungu Ibariki Tanzania:NoGodNo:
 
Back
Top Bottom