Serikali yetu ina mkakati gani na hawa wanauza mihadarati ya kiimani kwa jina la Yesu au ukristo?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Taifa linaangamia na kutengeneza jamii ya mataahira. Wakuu wangu wa serikali nawaheshimu sana lakini hapo mmekaa kimya. Kusema serikali haina dini mnamaanisha matapeli waliojificha kwenye imani ya dini mkono wa serikali ambao tunajua ni mrefu hauwafikii hawa matapeli na ambao asilimia kubwa wapo kwenye imani za kidini?
 
1721920413020.jpg
 
Hii miujiza ingekuwa inatoka kweli kwa Mungu tungekuwa taifa sifika duniani tukiongoza kwemye utengenezaji wa smart electronics space explorations na hata raslimali zetu za madini na bandari htungezifanyia kazk wenyewe kwa teknolojia inayotokana na ubongo wetu. Tumebaki na upumbavu tu wa miujiza feki. Where is my country heading into. Jamani hebu tufunguke kidogo. Tunachekwa sana huko nje. Tuna ma PhD ya makaratasi tu!
 
Hilo sio swala la serikali hilo ni suala la dini husika kuweka mikakati ya kuwashughulikia matapeli maana serikali haina dini.
 
Wajinga ni wengi hii nchi nilishangaa kuona miwatu inamsumjudia zumaridi ccm itakaa sana madarakani
 
Kwa hiyo unataka mwamposa asitishe kazi zake,utamlisha wewe? Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Hilo sio swala la serikali hilo ni suala la dini husika kuweka mikakati ya kuwashughulikia matapeli maana serikali haina dini.
Asante sana lakini dini zipi hizo? Dini is nowadays a private issue. Unaweza kulala usiku ukaamua asubuhi utumie biblia kujiita nabii mkuu. There is no controlling religious authority. Mambo haya yanatokea ndani ya nchi ndio maana nimeitaja serikali itupie jicho.
 
Mihadarati tena
Kumbe nini?

Ikiwa mtu anaaminishwa kwenye mitandao ya kijamii na mchungaji aliye-post picha ya nyumba kwamba “andika amen kesho utaamkia kwenye nyumba yako unayoimiliki” na anaandika kweli huku amelala kitandani kwake kwenye chumba kimoja alichopanga kuna uwendawazimu zaidi ya huu?
 
Hata wewe ni sehemu ya mkono wa serikali kama unataarifa zo zote kuhusiana na hilo nenda karipoti polisi.
Kinachoendelea huko motaani na kwenye redio za hawa matapeli wa kiroho kwani hawakijui? Everything is on air. Hakuna kificho. Utapeli uko hadharani kila mtu anausikia anapita pembeni! Unataka tena niende polisi kumripoti mtu anayesikika mitaani na redioni. What are you talking about????
 
Hilo sio swala la serikali hilo ni suala la dini husika kuweka mikakati ya kuwashughulikia matapeli maana serikali haina dini.
Taasisi za dini zina vyombo vya kisheria kuweza kuwadhibiti matapeli?
 
Kumbe nini?

Ikiwa mtu anaaminishwa kwenye mitandao ya kijamii na mchungaji aliye-post picha ya nyumba kwamba “andika amen kesho utaamkia kwenye nyumba yako unayoimiliki” na anaandika kweli huku amelala kitandani kwake kuna wendawazimu zaidi ya huu?
Mihadarati ni suala lolote linaloathiri akili. Siyo lazima iwe coccaine au bangi
 
Taasisi za dini zina vyombo vya kisheria kuweza kuwadhibiti matapeli?
Inatakiwa viongozi wa dini waweke taratibu za mtu kuendesha ibada na vigezo lakini pia wakubaliane dini zote kwa pamoja baadhi ya sheria zitakazowekwa kwasababu haiwezekani mtu akiwa na hela tu anaanzisha kanisa na hili ni tatizo kwa Christian dini inafanywa biashara.
 
Asante sana lakini dini zipi hizo? Dini is nowadays a private issue. Unaweza kulala usiku ukaamua asubuhi utumie biblia kujiita nabii mkuu. There is no controlling religious authority. Mambo haya yanatokea ndani ya nchi ndio maana nimeitaja serikali itupie jicho.
Mkuu mambo ya dini huwa yana mkanganyiko sana lakini kikubwa zikiwekwa sheria na taratibu hayo mambo yata pungua kwa kiasi kikubwa sana.
 
Taasisi za dini zina vyombo vya kisheria kuweza kuwadhibiti matapeli?
Kama wakifanya utapeli ndani ya taasisi zao wanaweza. NKwa mfano mtume au nabii amefungua kanisa lake halina ufungamano na taasisi kama catholic au baptist nani ana mamlaka ya kuuhukumu. Ni mtu ametafuta mbinu ya kuwatapeli watu akaamka asubuhi akasema jana Yesu alimtokea na leo anaitwa nabii mkuu. Mamlaka gani ya kikristo inaweza kumdhibiti mtu huyo??????
 
Hii miujiza ingekuwa inatoka kweli kwa Mungu tungekuwa taifa sifika duniani tukiongoza kwemye utengenezaji wa smart electronics space explorations na hata raslimali zetu za madini na bandari htungezifanyia kazk wenyewe kwa teknolojia inayotokana na ubongo wetu. Tumebaki na upumbavu tu wa miujiza feki. Where is my country heading into. Jamani hebu tufunguke kidogo. Tunachekwa sana huko nje. Tuna ma PhD ya makaratasi tu!
Sema hoja yako haina msingi..
 
Mkuu mambo ya dini huwa yana mkanganyiko sana lakini kikubwa zikiwekwa sheria na taratibu hayo mambo yata pungua kwa kiasi kikubwa sana.
Vyema sana asante but when will this come into effect?? Tuamke jamani. Juzi tu hapa Trump ameminya misaada watu wameanza kuli. Nchi tuliyojitawala for more than 50 years yenye rasslimali kibao kweli bado tulie lie . Hata mwanao umemlea ana miaka 50 bado tena ni tegemezi. Mhhhh!!
 
Back
Top Bottom