Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,418
- 4,031
Ni kweli tunahitaji watoto wote nchini wasome wapate maarifa ya kulijenga zaidi Taifa letu. Ni kweli kuwa siyo kila mmoja wao atahitajika afike Sekondari ndio awe na maarifa ya kujenga Taifa. Msingi Mkuu wa kuingia Sekondari ni ufaulu wa kutosha wa mitihani ya kumaliza shule za msingi.
Msingi wa pili ni uwepo wa vyumba vya madarasa vya kutosha vya kupokea kidato cha kwanza kila mwaka, waalimu, vifaaa nk. Hapa ndipo penye kujikita mada yangu. Sipingani na mawazo ya Serikali katika maamuzi ya namna inavyotatua changamoto za ujenzi wa madarasa, upatikanaji wa samani nk ila kwa nini ni ghafla na shuruti? Ghafla kwa maana:-
1. Wizara ya Elimu ina takwimu za kutosha kuwa, ni watoto wangapi watahitimu darasa la saba kila mwaka, je, kwa nini wasiwajibike kwa kutofanya maandalizi mwaka mzima? Walishirikishaje wananchi kuanzia Januari hadi Disemba ya mwaka husika?
2. Viongozi wakuu wa nchi yetu walipiga marufuku michango kuwa ni kazi ya serikali kujenga shule na madarasa,wananchi wanunue vitabu,uniforms na mambo madogomadogo! Hili lilikuwa ni wazo zuri sana endapo lingekuwa shirikishi zaidi. Ikumbukwe hapo hawakushirikisha wananchi/wazazi kwani walishazoea kuchangia ujenzi wa shule.
Je, nini kimepekekea upungufu unaosikika kila mahala wa madarasa? Hii ni ishara na viongozi wetu na sote tukubali sababu ni ile ya kuondoa ghafla michango muhimu ya maendeleo ya shule zetu toka kwa wananchi. Kama serikali imebadili ilani ya elimu bure,basi viongozi wakuu watoe tamko ili michango irejeshwe kwa utaratibu mzuri na wazazi/wananchi wajue.
Mwisho
Mimi kama mdau wa Elimu, ninashauri Kamati za shule, halmashauri za Wilaya, Wizara ya Elimu ziratibu vyema vipaumbele vya mahitaji ya uboreshaji wa elimu katika maeneo yao mapema ili pasiwepo na ghafla hizi za Januari za kila mwaka. Pia,Taasisi hizi zijikite kuona ni namna gani mtoto anayemaliza darasa la saba anaweza kusaidiwa kushiriki shughuli za kujenga Taifa.
Ninaamini siyo lazima kila mhitimu wa darasa la saba aende sekondari. Tusilazimishe hata wasio na sifa za kutosha waende sekondari huku tukibinya wazazi wajenge madarasa kwa vilaza ambao wataambulia 0 form 4. Na wakirudi kijijini wanaanza kutafuta kazi ambazo ziliwastahili walipomaliza darasa la saba.