Serikali za Mitaa tungeni Sheria kuokoa vizazi hivi

Serikali za Mitaa tungeni Sheria kuokoa vizazi hivi

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
748
Reaction score
367
Mkoa wa Dar es Salaam nimoja kati ya mikoa yenye kitu kinaitwa shughuli

Hii kitu hua ni familia fulani inaamua kuweka sherehe maalumu hua zina majina mfano beseni, arobaini, kumtoa mwali na majina mengine wazaramo wanajua sana hii kitu.

Ukiangalia maudhui ya matukio haya hua sio mabaya wanajamii wanachangiana wanafurahi pamoja n.k

Ila sasa uhalisia wa tukio hili huaga lina vituvingi ndani yake hasa kwenye vipengele vya burudani na kutoa zawadi. Watu hua wanacheza uchi, wanawacheza wakiwa uchi hukuwakiwainamia watoto n.k hii kitu inaathiri sana watoto wadogo wanajikuta wanakua katika misingi hiyo na mwisho wanakua (vyura) walioshindikana.

S/ za mitaa

Acheni kukaa tu ofisini kusubiri wanaenda kuomba kazi mchukue 2000 zao za barua au mnasubir watu wauziane nyumba mchukue %?

Sheria inawapa mamlaka ya kutunga sheria ndogo za kuendesha mitaa yenu sasa mbona hakuna utaratibu wa kuokoa vizazi hivi? Kwanini shughuli zao wasifanyie ukumbini huko wacheze uchi wakiwa wakubwa tu?

Mkigombea uongozi nendeni mkafanye kazi itakayo isaidia jamii msikae ofisini kama misukule. Wekeni miradi ya kijiji hata kuuza maua nje hapo. Angalia picha hizo shughuli ya beseni huko Kiwalani. Hao ni watoto wadogo sana.

Screenshot_20210718-232444.jpg


Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app

Screenshot_20210718-232412.jpg
 
Back
Top Bottom