TF
Nadhani huyu anatania tu. Kama yuko serious, ningemshauri aombe Mungu sana ili amuumbie wa kwake kama alivyo sema FA hapo juu. Mwanamke aliye tayari kutimiza masharti ambayo yanakinzana yenyewe mbona kazi!
Imagine kwa mfano mwanamke atakayetimiza kigezo hiki:
13: "You should be ready and willingly to respect, obey and observe my directions,commands,wills,wishes and ideas without any strong criticism." halafu hapo hapo aweze kutimiza hili:
14:"You should be courageous girl." anahitaji kuwa programmed na Muumba tu. Binadamu hawezi kufyatua mtu mwenye "features" zote azitakazo huyu bwana.
Tumtakieni kila la kheri.
ANGALIZO: Wadada watakaoweza kuingia kwenye mchujo na hatimaye kuibuka kidedea mjiandae kwa maisha ya mateso na msalaba hadi kifo kitakapowatenganisha!