Serious: Nifanyeje?

.......TIBA kama alivyosema KKS......kama ni tafuta "kibiyonce" wako jivinjari nae pembeni kidogo ya mji kwa siku 2 tu.....mind u usiache pc...pc is life.....
Huu ushauri nahisi unanishinda... Lakini asante kwa ushauri mkuu
 
Hapa invisible kazi ni moja tuu.
Hela iko siku zote, ndugu wa kweli wataelewa, jamii forum inaweza kuendeshwa na ma MODS wengine kina mzee wa kiminyio MELO.....

Jambo la mbolea ni wewe kufunga virago na kwenda nje ya miangaiko ya mjini.
siku mbili tatu zitakutosha. tafuta SIM card nyingine wape number watu wenye umuhimu na uangalie message za muhimu every 6 hours.
Utakuja kufa au kuumwa ukose vote....
 
Invisible

Take some time off kama ulivyoshauriwa, nenda maeneo mapya ambayo hujawahi kuyatembelea, tumia muda mwingi nje ya nyumba. Maeneo kama beach, mbuga za wanyama na sehemu kama hizo.

Usiache familia yako nyuma kwani kwa kufanya hivi kutakufanya uiwaze hivyo kutokupata pumziko unalostahili. Cha muhimu mueleze mwenzio kwamba unahitaji utulivu na liwazo lake kuliko wakati mwingine wowote.

Kunywa maji mengi sana, kula nyama ya kuku kwa wingi hasa mchemsho wa kuku wakienyeji. Kuku wana antioxidant kwa wingi, ambazo ni muhimu kuondoa free radicals mwilini mwako kutokana na stress. Pia kula matunda na mbogamboga kwa wingi.
 
SteveD na Yo Yo, msiharibu wala kujaribu kudiverge hii thread tafadhali. Mnajua pa kwenda.
 
SteveD na Yo Yo, msiharibu wala kujaribu kudiverge hii thread tafadhali. Mnajua pa kwenda.

Mama vijana wanasuggest solutions ambazo zimekuwa tested and proven, yote hii ni katika kumsaidia mwenzetu. Sasa akienda akajichimbia mahali peke yake si ndo hata madepression yanaweza kumvamia? atakuwa anawazia mambo mengi sana, bora awe na mwenzie wa kum keep busy, apate vitu adimu ambavyo huwa havipati mara kwa mara!
 
Hiyo ni burnout Invisible. Fanya mazoezi kaka baada ya wiki moja wewe mwenyewe utashangaa.
 
Kijana unatakiwa uwe na serious talk na mama watoto kwa uzoefu mara nyingi matatizo kama haya yanaanzia nyumbani anatakiwa akupe space unapokuwa nyumbani kama hatoweza kukusaidia then do what you think is right but make you don't hurt your children.

SAHIBA.
 
watu hapa wanajuana, mbona ongea na mama watoto ama tafuta totoz, kwani kasema yeye ni mkaka.

Invisible unaitaji mapumziko, kama unavyowaza mwenyewe, siku tatu, wacha simu nyumbani,usichukue chochote zaidi ya pesa ama card ya bank na nguo,nenda sehemu mpya kwako,lakini hiwe na watu wengi,maana kukiwa hakuna action,mawazo yatakuwa yanakuja sana so kutakuwa hakuna mapumziko, nakushauri nenda sadani tanga,kule kwenye mbuga na bahari.
mapumziko mema!
 
Ndugu yetu Invisible pole sana,
Kwa haraka haraka tatizo lako ni "Stress", kila mwanadamau at some point ana stress ila viwango hutofautiana.
mara nyingi sababu kuu za stress ni
•pressure ya kazi au shule,
•hofu ya kutishiwa maisha,
•hofu ya kutokuwa na pesa,
•migogoro kazini au nyumbani,
•divorse,
•kukosa kazi,
•kutokuridhika na hali ya kikazi au kimaisha.

Utajuaje una stress;
•Uchovu unaopitiliza
•Msongo wa mawazo
•Kukosa hamu ya tendo la ndoa
•Anxiety (sijui niitaje kiswahili)
•Kukosa apetite ya kula
•Kutokuwa mwangalifu kwa baadhi ya mambo(lack of concetration)
•maumivu ya shingo,mgongo,kichwa na misuli.
•Kwa wanawake kukosa hedhi
•kuwa na tabia za ajabu ajabu mfano ukali ukali, kununa ovyo

Baadhi ya vitu unavyoweza kufanya kuondoa stress:
•Kufanya mazoezi laini-mfano kutembea hata dakika 30
•kugawa baadhi ya majukumu (delegating)
•Punguza pombe, kahawa
•Kula balanced diet
•Kuwa na muda wa kutosha wa kupumzika
•kuwa na muda wa kushare feelings na mtu wa karibu eg mke au mume ; mweleze huyu mwenzi unavyojisikia,hofu zako,matarajio , mweleze akusaidia baadhi ya mambo.
•Pata muda tulizu wa kujichunguza binafsi- walau dakika 50 kwenye bustani huku ukiwa na utulivu wa kutosha.
•Pata muda wa kuzungumza na Mola wako na kumwomba akusaidia kuprioritise mambo.
•Ukiweza weekeend mchukue mkeo/mumeo mkae mbali na watoto muongee na kupumzika beach au mbali na nyumbani ambapo kila saa ni hodi,hodi mara wageni, mara kadi ya mchango ,mara ujenzi wa mitaro- take time nyie wawili muende mbali mkafanyiane massage.


Baadhi ta stree huwa mbaya sana hadi mtu huweza kuanguka ghafla, akili kusimama kwa muda, kupoteza kumbukumbu n.k
Na wengine hufikia kupewa anti-anxiety pills( Diazpem) lakinini vidonge hivi si vizuri kwani vitakulazimu uvitegemee kila mara. Miili tatu imeumbwa ifanye kazi kwa kiasi, ipumzike kiasi kwa hivyo ni vyema tuweke vipaumbele- tunatafuta pesa ndio lakini mwili unahitaji kurecharge, tuipende miili yetu ili akili zetu ziendelee kuwa active.
Wish you Quick recovery Invisible.
 
Invisible! You are visibly exhausted...

shut off for a week, be selfish for once, you only live once and even if you die now, hizo kazi atapewa mwingine na hata JF pia itaendelea

For once think about you and those you love dearly... forget everything else

Ndugu yangu ukifa Kaburi lako halitaandikwa XXX of XXXX bin invisible bin JF bin four conpanies bin etc.. bin etc

Everything living is replaceable ndugu
 
Kaka chukua Vacation tuu, waambie hao waliokuajiri kwamba samahani, maana ni Bora kuwahi kutulia sasa hivi ili uje ufanye kazi vizuri. Yaani nenda mahali ambapo familia wanaweza kukutembelea, ila kaa mbali na simu na Computer.
 
Kaka nafikiri umepata ushauri wa kutosha sasa unatakiwa kufanya maamuzi ya haraka na si vinginevyo.
 
Mkuu invisible,
Pole sana lakini hapo ndo mtu unaweza kuprove kuwa uko so addicted to JF. Nadhani all that is largely contributed na JF involvement yako. Anyways angalia all you can ili uweze kubalance yote but remember we need you here badly.
 
Itabidi mkiombwa JF kuwa down for maintenance mtukubalie tu

Kama itafungwa kwa ajili ya kuboreshwa, hiyo ni neema, nenda kapumzike mkuu. haitatusaidia sana iwapo utajilazimisha kufanya kazi kwa ajili ya kuifanya JF iwepo halafu baada ya muda, ukaziidiwa kiasi cha kuiathiri JF kwa muda mrefu
 
Mkuu Invisible ni bora upumzike, unaweza kuja kujisabaishia mtatizo makubwa zaidi baadae. Nadhani hayo makampuni yanajua wewe ni binadamu. Hivi ikitokea ukapata tatizo la kibinadamu ambalo huwezi fanya kazi ndio watasimamisha nao kazi zao?. Waeleze ukweli kuwa umeshauriwa na daktari kupumzika, nadhani wakiona hilo watakubali. Kuhusu familia kama wengine walivyoshauri ni vizuri kuwa nayo huko utakapoenda kupumzika, familia ina raha zake.

Mwisho, hivi unakutanaje na madaktari wakati hauonekani (Hebu jitokeze, simama, mbele ya watu...)
 

Nakubaliana na wewe kabisa,,,, he needs to be away for a while,,,, mahali ambapo ata relax,,,,, somewhere far,,,, iambie familia yako ukweli,,,, am sure wanakupenda watakuelewa tu. Wazo la kutafuta demu sikubaliani nalo,,, huko ni kuongeza matatizo bure. Kamwe usijaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…