Ndugu yetu Invisible pole sana,
Kwa haraka haraka tatizo lako ni "Stress", kila mwanadamau at some point ana stress ila viwango hutofautiana.
mara nyingi sababu kuu za stress ni
•pressure ya kazi au shule,
•hofu ya kutishiwa maisha,
•hofu ya kutokuwa na pesa,
•migogoro kazini au nyumbani,
•divorse,
•kukosa kazi,
•kutokuridhika na hali ya kikazi au kimaisha.
Utajuaje una stress;
•Uchovu unaopitiliza
•Msongo wa mawazo
•Kukosa hamu ya tendo la ndoa
•Anxiety (sijui niitaje kiswahili)
•Kukosa apetite ya kula
•Kutokuwa mwangalifu kwa baadhi ya mambo(lack of concetration)
•maumivu ya shingo,mgongo,kichwa na misuli.
•Kwa wanawake kukosa hedhi
•kuwa na tabia za ajabu ajabu mfano ukali ukali, kununa ovyo
Baadhi ya vitu unavyoweza kufanya kuondoa stress:
•Kufanya mazoezi laini-mfano kutembea hata dakika 30
•kugawa baadhi ya majukumu (delegating)
•Punguza pombe, kahawa
•Kula balanced diet
•Kuwa na muda wa kutosha wa kupumzika
•kuwa na muda wa kushare feelings na mtu wa karibu eg mke au mume ; mweleze huyu mwenzi unavyojisikia,hofu zako,matarajio , mweleze akusaidia baadhi ya mambo.
•Pata muda tulizu wa kujichunguza binafsi- walau dakika 50 kwenye bustani huku ukiwa na utulivu wa kutosha.
•Pata muda wa kuzungumza na Mola wako na kumwomba akusaidia kuprioritise mambo.
•Ukiweza weekeend mchukue mkeo/mumeo mkae mbali na watoto muongee na kupumzika beach au mbali na nyumbani ambapo kila saa ni hodi,hodi mara wageni, mara kadi ya mchango ,mara ujenzi wa mitaro- take time nyie wawili muende mbali mkafanyiane massage.
Baadhi ta stree huwa mbaya sana hadi mtu huweza kuanguka ghafla, akili kusimama kwa muda, kupoteza kumbukumbu n.k
Na wengine hufikia kupewa anti-anxiety pills( Diazpem) lakinini vidonge hivi si vizuri kwani vitakulazimu uvitegemee kila mara. Miili tatu imeumbwa ifanye kazi kwa kiasi, ipumzike kiasi kwa hivyo ni vyema tuweke vipaumbele- tunatafuta pesa ndio lakini mwili unahitaji kurecharge, tuipende miili yetu ili akili zetu ziendelee kuwa active.
Wish you Quick recovery Invisible.