Serious!!! Usalama wa nchi unatia mashaka-Nchi iko uchi!!

Serious!!! Usalama wa nchi unatia mashaka-Nchi iko uchi!!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Nimelitafakari hili swala la madawa ya kulevya hapo JK Nyerere Airport, na kuliwazua tena.
Lakini mwishowe naona hali ya kutisha kidogo.

Kwamba imekuwa kawaida kwa madawa kupitishwa hapo "by design" na siyo "by chance", hili limenipa kigugumizi cha mawazo.

Nchi iko uchi.

Kama wale waliopewa dhamana na taifa hili kulilinda tena kwa kiapo, ndio wakaweza kununuliwa na mtandao wa drug lords, hapo napata wasi wasi kwamba, is this the tip of the ice berg?

Uwanjani JKNIA kuna Idara karibu zote nyeti za dola
Kuna Polisi wa kawaida
Kuna Polisi wa kuzuia madawa ya kulevya
Kuna Usalama wa Taifa
Kuna uongozi wa Kiwanja kwa maana ya Wizara ya Uchukuzi/Tanzania Airports Authority(TAA)
Wafanyakazi wa Ndege zinazoruka

Kinachonishangaza ni kwamba hao wote wameweza ku-collude katika hili la madawa ya kulevya, na waka fanya uovu ambao kimsingi ni hujuma.Tukumbuke kuwa Idara hizi nyeti zote zina mamlaka tofauti kila moja, na answerability ni huko huko walikopewa tasks za kufanya hapo kiwanjani JKNIA.
Hapo ndio wasi wasi wangu mkubwa.

Nchi iko uchi.

Je tujiulize , ni kitu gani zaidi kimekwisha kutoka au kuingia, kitu ambacho ni haramu kwa nchi kiusalama?

Tunachokiona hapa kwetu sasa hivi ni matokeo ya kuwa na serikali corrupt na iliyoamua kupuuzia uadilifu. Mojawapo ya zao la corruption katika state ni kukua kwa matumizi ya nguvu kwa watawala dhidi ya watawaliwa. Hali hii ikikomaa hufanya watekelezaji wa amri za ukandamizaji (polisi, usalama nk) kuhisi wao ni washikadau muhimu wa serikali husika. Hivyo kujisikia wapo salama katika group la untouchables! Mathalan kwenye nchi kama yetu ambapo mpaka kiongozi mkuu wa nchi ni mshukiwa katika list ya mafisadi, ni aghalabu kupatikana idara zozote zilizo hai kwani uwajibikaji huwa umezikwa toka juu mpaka chini, kwa maana halisi ya "nani atafuatilia kama mpaka mkuu ameharibika?"

Kufikia hapa niwazi kuwa Watanzania wengi wanajulikana kuwa na bei katika lolote! Katika mazingira haya ni rahisi mtu yeyote kupitisha chochote ili mradi afike bei tu ya kuachiwa njia!

Siwezi kusema au kukisia, lakini nina uhakika hii nchi imejaa majasusi wa nchi nyingine , kwa kuwa ni rahisi sana kupita, imeshaingiza vitu vya hatari vingi sana kwa kuwa hata ukaguzi unaendeshwa kutafuta dili tu. Ikifikia hapa huwa ni rahisi hata maadui wa nchi kujipenyeza na kuratibu zoezi lolote haramu ndani ya nchi kwani watapitisha vifaa vyao vyote bila tabu na wataondoka bila shida.

Kama ulivyosema ni kweli nchi iko uchi. Na mbaya zaidi ni uchi kwa kiwango cha kutishia amani uhai wa taifa letu kutoka kwa maadui zetu. Na kama tusipochukua uamuzi sahihi basi tukae mkao wa kutegemea lolote. Kama siyo leo basi kesho.
 
wewe unafikiri mchezo jamaa wamarekani wanajua ishu za hapo uwanjani kutoka A-Z ndiyo maana hata alipokuja rais Obama ilibidi wao ndiyo wachukue uskani wa uwanja huo maana wabongo mnafanya mzaha hata kwa usalama wa nchi, nyambafu setu sana sisi watz!
 
Unategemea nini kama member wa Royal Family ndio hao druglords? Mzee atasema lolote?
Namwonea huruma sana Ndg Mwakyembe maana ni Yatima ktk vita hiyo.
 
Nimelitafakari hili swala la madawa ya kulevya hapo JK Nyerere Airport, na kuliwazua tena.
Lakini mwishowe naona hali ya kutisha kidogo.

Kwamba imekuwa kawaida kwa madawa kupitishwa hapo "by design" na siyo "by chance", hili limenipa kigugumizi cha mawazo.

Nchi iko uchi.

Kama wale waliopewa dhamana na taifa hili kulilinda tena kwa kiapo, ndio wakaweza kununuliwa na mtandao wa drug lords, hapo napata wasi wasi kwamba, is this the tip of the ice berg?

Uwanjani JKNIA kuna Idara karibu zote nyeti za dola
1.Kuna Polisi wa kawaida
2.Kuna Polisi wa kuzuia madawa ya kulevya
3.Kuna Usalama wa Taifa
4.Kuna uongozi wa Kiwanja kwa maana ya Wizara ya Uchukuzi/Tanzania Airports Authority(TAA)
5.Wafanyakazi wa Ndege zinazoruka

Kinachonishangaza ni kwamba hao wote wameweza ku-collude katika hili la madawa ya kulevya, na waka fanya uovu ambao kimsingi ni hujuma.Tukumbuke kuwa Idara hizi nyeti zote zina mamlaka tofauti kila moja, na answerability ni huko huko walikopewa tasks za kufanya hapo kiwanjani JKNIA.
Hapo ndio wasi wasi wangu mkubwa.

Nchi iko uchi.

Je tujiulize , ni kitu gani zaidi kimekwisha kutoka au kuingia, kitu ambacho ni haramu kwa nchi kiusalama?

Nchi iko uchi.
ongezea
6. polisi wa siri nao wapo hapo
Ila ndg. yangu Masopakyindi, tatizo liko kwa watawala wetu.
Sio kwa wasambazaji na wauzaji wa madawa ya kulevya.
Hakuna kukwepesha Baba anabeba lawama hata kama hahusiki
Hivi mpaka sasa ni mangapi mazito yanayoliangamiza taifa, watawala
wameyakomalia kuyapatia ufumbuzi, jibu ni hakuna. Ninachokiona ni
kupambana na mambo ya siasa wakati nguvu kazi inaangamia kwa
madawa ya kulevya, ufisadi sasa ni wimbo.

Piga picha ile nguvu iliyotumika kuwanyamazisha Wanamtwara.
Ingetumika kuwasaka wasambazaji na wauza madawa ya kulevya,
dunia ingetusifu sasa tumekuwa kichekesho mbele za wanaume
wenzetu. Hebu fikiri nguvu hizo hizo zingetumika kupambana na
ufisadi hali ingekuwa shwari na maendeleo makubwa zaidi ya
haya yaliyofikiwa yangeonekana.
Tumekalia siasa tu, hata kuiga kwa walioendelea tunashindwa.
SUALA LA MADAWA YA KULEVYA NI AIBU KWA TAIFA LETU
 
chezea watoto wa mjini nyie!!! ndio maana hata kagame naye eti anatingisha kiberiti kama njiti zimo.. ilitakiwa kagame awe kishaomba radhi kama tunauwezo wa kuthubutu!!!
 
Wewe unaona la madawa tu? Mtazamo finyu sana.
Funguka mkuu, kwa yale unayoyaona.
Pale JNIA hii ya kupitisha madawa , ina maana kuna security breach, na kama kuna hilo tatizo basi JKNIA is no longer secure-kitu chochote chaweza kupita pale, hata bomu la nuclear!

All this from our own personell ambao si mgambo, la hasha bali vijana waliopitia mafunzo ya kazi zao.
Na je supervisory procedures ziko wapi?
Na hilo ni katika ngazi zote hadi kufikia apex ya kila idara iliyopo pale JKNIA.
Na leo Kagame akisema atatufanyizia, naanza kuona mwanya!
Inasikitisha!!
 
Mkuu wewe unashangaa unga!!!! ambao unafichika, hujiulizi kuhusu twiga na pundamlia waliopanda ndege pale KIA na bado ndo tunaambiwe eti ni safe kwenye suala la unga..
 
We are exposed for everything...ni muda tu tutaipata kitu ya kutosha
 
Wewe unaona la madawa tu? Mtazamo finyu sana.

Enrich the debate dont just criticize. IF you were of a broader scope you wud have complemented on the topic!!!!!

What are your insights on issues regarding state security???
 
Kama serikali imewalea kwa kuhifadhi maovu yao kwakung'oa kucha basi na wao wameona wale kiivyo pasipokujua wataitumbukiza Taifa shm gani?
 
Boresheni mishahara wacheni kulalamika mtu unamlipa laki moja kwa mwezi maisha magumu unategeme nini?leo mtu anakuja na 3m utaiwacha wakati hiyo hela ufanyekazi miaka kibao ndio utie mkonono mabadiliko maisha bora kwa kila mtz uzalendo utakuwepo
 
Tukomae tu maana hata usalama wa dunia na kizazi kijacho unatia shaka.
 
kiongozi,ivi uliamini kabisa tanzania ina "usalama wa taifa"?
watu wanaochaguliwa kwa interview za kimagumashi tu walio wengi?
tena hawa hawa wanaojichoresha fesibuku?
awa vijana kina "yahaya" tunaowaona wanavoshoboka mtaani,baa nk?
awa wanaopiga madili ya kubomoa vyama vya siasa?mana naona apa ndo kazi yao wanayoiweza zaidi🙂

hii nchi ilishakua uchi kitambo tu ata kabla jk hajatawala,ingawa baada ya jk ndo wamekufa kabisa

mara mia tuishi kama wasomali tu:tape:

ebu niishie apa kucha zangu nazipenda sana...na uzuri wa dunia bado nataka kuuona!!
 
Kusema ukweli nashindwa kabisa kuelewa taifa hili limepatwa na nini haingii akilini mambo ya ajabu kabisa yanafanyika bila vyombo vyetu vya usalama kufahamu, mara magari kupitisha wakimbizi.mara afisa wa jeshi atoroka na kusemekana alikuwa mnyarwanda,mara gari la polisi lakamatwa na bangi,madawa ya kulevya, nyara za taifa nk hao usalama wetu wa taifa kweli wapo? Pengine ule utaratibu wa watoto wa wakubwa kupewa sekta zote nyeti wameamua kuwalinda vigogo maana pia inasemekana hzo biashara haramu kwa taifa ni za wakubwa serikalini au watu wenye ushawishi mkubwa kwa viongozi wetu.
 
kiongozi,ivi uliamini kabisa tanzania ina "usalama wa taifa"?watu wanaochaguliwa kwa interview za kimagumashi tu walio wengi?tena hawa hawa wanaojichoresha fesibuku?awa vijana kina "yahaya" tunaowaona wanavoshoboka mtaani,baa nk?awa wanaopiga madili ya kubomoa vyama vya siasa?mana naona apa ndo kazi yao wanayoiweza zaidi🙂hii nchi ilishakua uchi kitambo tu ata kabla jk hajatawala,ingawa baada ya jk ndo wamekufa kabisamara mia tuishi kama wasomali tu:tape:ebu niishie apa kucha zangu nazipenda sana...na uzuri wa dunia bado nataka kuuona!!
Mkuu nakubaliana nawe.Kuna tatizo hapa.Kama tunachoona ni trela, basi hii si trela nzuri.Lama walinzi wa usalama wa nchi wanaweza ku-collude na kuuweka usalama wa nchi rehani, basi kodi tunazotoa ni za bure.
 
Uadilifu uliondoka na baba wa taifa muda huu ni wa Chukua Chako Mapema (Ccm) ana Sema Ule(SU)
 
Back
Top Bottom