juve2012
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 3,343
- 2,040
Suala la madawa mkuu Masopakyindi litakupa presha tu kwa sababu uwezo wa kulitatua haupo kwa mtu mmoja,ni lazima dunia nzima ihusike.Utakaposema unapambana na hiyo kitu,ujue unapambana na akina nani duniani(sio Tanzania tu).Hii ni biashara ambayo kuna wateule kwao ni halali kuifanya,wengine mliobakia nje ya system mnajengwa kuwa negative nayo ili msiingilie njia kuu za uchumi za "wajanja",na hili linawezekana kwa vile dunia ya sasa inajali "faida ya fedha",bila kutazama njia zinazotumika kuipata hiyo fedha.Hatuna tathmini tena ya kujiuliza kipi chema na kipi kibaya.Siku hizi kile kinachozalisha faida ya pesa ndio chema.Nenda U.S kachunguze ni taasisi gani na watu gani wanaendesha hii kitu,utaelewa ukubwa wa tatizo hili.Unaposema unataka kupambana na hii kitu,ujue kwamba unaanzisha vita dhidi ya taasisi kubwa na watu mashuhuri sana duniani.Unapowasikia wakijifanya kukemea hadharani ujue ni "smokescreen" tu!dunia ya leo imejaa upuuzi ambao ukituliza kichwa ukatafakari,utaona tu gharika inakuja tena ila tu ni kwamba huenda Mwenyezi Mungu anatafuta kwa shida Nuhu mwingine na wanyama wa kuingiza kwenye safina!Maana yangu ni kwamba kabla ya kufikiri kukomesha drugs,inabidi uanzie mbali sana hiyo vita.Unahitaji jamii positive itakayokusapoti,sio hii ya wajasiriamali wa kila kitu chenye harufu ya fedha.