Seriously nahitaji msaada wako/wenu

mwananyiha

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2008
Posts
248
Reaction score
43
Ndugu wanajf baada ya kutafuta ajila kwa mda mrefu na kukosa nimeamua kujiajili kwa kufungua duka dogo la hardware. Nimeshapata tin na leseni. Changamoto ninayoface ni kuwa mtaji nilioanzia ni kidogo kulingana na aina ya biashara hivyo kuishia kupata pesa ya kulipa pango tu kwani vitu vingi wateja wanahitaji sina. Nimejaribu kutafuta kuomba mkopo kwa ndugu na jamaa imeshindikana na bank ni mpaka wanichunguze kwanza kwa kipindi maalum kama yalivyo mashart ya bank. Kutokana na hali hiyo naomba kwa yeyote mwenye duka kubwa la hardware dar niingie naye mkataba ili niwe nachukua bidha kwake na kuuza kwa commission au yeyete anaweza kunisaidia kurescue situation. Natanguliza shukrani mbarikiwe sana.
 

Hili duka liko wapi? Njia nyingine ya kuraise capital ni kumkaribisha mtu awe partner, uko tayari kwa ajili ya hili?
 
Hili duka liko wapi? Njia nyingine ya kuraise capital ni kumkaribisha mtu awe partner, uko tayari kwa ajili ya hili?
Mkuu nipo tayari ni namna tu ya kukubaliana ktk mkataba.
 
Dah, Mkuu hizo ndo Changamoto za Biashara hupaswi kukata tamaa ila kusonga Mbele, Vipi ndugu hawataki kusaidia? Ila ungekuwa unahitaji Michango ya Haurusi wemgetoa kwa wingi kabisa, That is why nachukia sana Kuchangishana kwenye Harusi badala ya Vitu muhimu kama Hivi

Ndugu wengi un akuta nao wamejaa wivu na unafiki wa hali ya juu, na kama Ndugu wangekuwa wanachangisha kwa ajili ya Mitaji kama wanavyo fanya kwenye harusi tungekuwa mbali sana,
 
Biashara ya hardware inahitaji mtaji mkubwa sana na ili iweze kukulipa location ya Hilo Duka ni muhimu sana..Kama utakua na mtu atakaeweza kukudhamini maduka mengi ya hardware ya jumla yanatoa mzigo kwa mali kauli cha muhimu ni uaminifu na huyo mtu wa kukudhamini nadhani hii ndio njia itakayoweza kukusaidia kufika unapopataka
 
Kwanza kabisa inavyoonekana wewe sikujui, lakini kwa mujibu wa maelezo yako inaonekana wewe ni mtu unayependa kupata faida kwa haraka au kwa maneno mengine, kukuza biashara katika muda mfupi wakati umeanza kidogo. Wewe unachotakiwa kufanya sasa si kutafuta duka kubwa ili wakupe bidhaa ule commision, unachohitaji ni kuvumilia hicho kipindi ambacho benki watakuchunguza ili wakupe mkopo, maana kama unashindwa kuvumilia hicho kipindi cha kuchunguzwa, utaweaje kuvumilia hizo commission ndogo ndogo mpaka zikusaidie kukuza duka lako? So wewe vumilia uchukue mkopo benki uwe huru zaidi
 
Mkuu sina nia hiyo ya kupata faida ya haraka. Lakini kadri siku zinavyokwenda kuna gharama za uendeshaji kama pango,umeme ulinzi hata mhusika kupata mlo wa mchana hivi vyote havitegemei unapata kiasi gani. Kuhusu banki wanavyo kuchunguza wanaangalia ni kiasi gani cha cash unaweka na kutoa na kwamba unakua kwa kiasi gani? Kama mwenendo wako ki cash si mzuri unaweza usipate. Asante.
 
Mkuu nashukru kwa kunitia moyo.
 
Mkuu nashukru sana kwani una uelewa mzuri wa aina hii ya biashara nitahitaji zaidi msaad wako.
 

yeah ofcoz.watu wanahusudu sana sherehe kuriko mambo ya maendeleo hii kitu inanikera sana ndo maana sichangii ovyo miharusi kwani hyo miharus yao inapalilia umaskini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…