mwananyiha
JF-Expert Member
- Mar 11, 2008
- 248
- 43
Ndugu wanajf baada ya kutafuta ajila kwa mda mrefu na kukosa nimeamua kujiajili kwa kufungua duka dogo la hardware. Nimeshapata tin na leseni. Changamoto ninayoface ni kuwa mtaji nilioanzia ni kidogo kulingana na aina ya biashara hivyo kuishia kupata pesa ya kulipa pango tu kwani vitu vingi wateja wanahitaji sina. Nimejaribu kutafuta kuomba mkopo kwa ndugu na jamaa imeshindikana na bank ni mpaka wanichunguze kwanza kwa kipindi maalum kama yalivyo mashart ya bank. Kutokana na hali hiyo naomba kwa yeyote mwenye duka kubwa la hardware dar niingie naye mkataba ili niwe nachukua bidha kwake na kuuza kwa commission au yeyete anaweza kunisaidia kurescue situation. Natanguliza shukrani mbarikiwe sana.