DOKEZO Service Road Kuelekea Stendi ya Magufuli Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho

DOKEZO Service Road Kuelekea Stendi ya Magufuli Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

spyboss

Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
45
Reaction score
69
Wakuu habari za mchana.

Serikali yetu inapambana sana kuwaletea wananchi wake maendelea. Naipongeza kwa kazi nziri.

Pamoja na hayo nna jambo ambalo limenifanya niandike uzi huu. Kuna service road zimejengwa ili kusaidia kuingia Magufuli Stendi na Stendi Ndogo ya Daladala Hapa mbezi. Ukiwa unatokea Ubungo utaingia kushoto halafu utafuata hiyo barabara iliyojengwa hadi kuingia stand lkn utagundua kwamba upande wa kushoto mwa hiyo barabara kuna bonde kubwa ambapo watu wako chini wanafanya biashara hususan wale wanaoelekea Msigani au Kinyerezi.

Kuna siku tutapata janga kubwa sana kama ukingo wa maana hautawekwa kuzuia magari iwapo lolote litatokea.

Nawasilisha
 
Daraja liunganishwe hadi ndani stendi siyo unapanda unashuka then unavuka Tena ktk zebra
 
Mbaya zaidi ni hakuna kingo za kuzuia endapo kutatokea la kutokea. Lakini tuwapongeze japo kwa hili, Mbezi imekuwa vizuri kwa sasa, hasa katika kupunguza foleni.

Rai yangu ni moja, kule chini kuelekea Kinyerezi wapanue barabara, bado kuna msongamano sana.

Mbili, kuwe na recreation area jamani. Hivi kwa nini watu hawawazi maeneo mazuri yenye vivuli na viti, majani yanayohudumiwa vizuri kwa ajili ya wasafiri na watu wanaotaka kucheza na watoto wao. Sisi wengine hatupendi kwenda bar kwa ajili ya mazungumzo na marafiki zetu.
 
Back
Top Bottom