BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Baadhi ya barabara ambazo naweza kuzitumia kama mfano licha ya kuwa na tija, ni kipande cha Service road kilichopo Tabata Mwananchi, kipande cha Mbezi beach (kituo cha Shule hadi kituo cha Makonde pamoja na kipande cha Africana), njia hizi zimekuwa hatari kwa usalama wa wananchi wanaoendesha vyombo vya moto hata kwa watembea kwa miguu.
'Service road' zinaoneka kuwa njia hatarishi kutokana na kutokuwa na alama muhimu barabarani ambazo utakiwa kuzingatiwa kama zilivyo njia rasmi, mfano alama za zebra ambazo utumika kama sehemu ya watembea kwa miguu kuvuka.
Hatari hiyo kubwa hasa inaongezeka zaidi mida ya usiku ambapo wandesha vyombo vya moto wengi wao wanakuwa na mwendokasi bila kuzingatia usalama wa watembea kwa miguu.
Changamoto nyingine inayochangia uwepo wa hatari kubwa baadhi ya service road kuna maeneo 'bodaboda' wameanzisha vituo (parking) jambo ambalo linaongeza uhatari.
Hatari katika njia hizo inakuwa kubwa kwa sababu Traffic fokasi (focus) yao kubwa inakuwa ni kwenye njia rasmi huku service road zikendelea kutumika vibaya.
Wito wangu kwa mamlaka, kwa kuwa tayari wapo watu wamepoteza maisha na wengine kupata ulemavu kutokana na 'service road', nashauri mamlaka kuongeza usimamizi katika njia hizo, ikibidi katika njia za aina hiyo ambazo wakati mwingi utumika kama njia rasmi ziwekewe alama muhimu ikiwemo zebra pamoja na matuta ili kupunguza ajari zinazoweza kuzuilika.
Pia mamlaka zifuatilie kwa ukaribu maeneo ya 'service road' ambapo bodaboda wameamua kuweka vituo vyao waone kama ni salama, ikibidi baada ya ufuatiliaji huo waelekeze kwa utaratibu rafiki bodaboda kupaki katika maeneo ambayo yataonekana kuwa salama.
Kwa kuyafanya hayo tutaokoa maisha ya wengi, lakini hali iliyopo ikiendelea uenda watu wataendelea kupata ulemavu na pengine wengine kupoteza maisha.