Mkuu ukipiga selfie nyota zinakuwa hazijaendana na nani? Au yule unayekuwa unamuwaza 😀😀😀😀
Hapa mada zimechanywa mbili tayari.
Lakini kwa swali lako ukipitia hii comment ya Apollo utaelewa 👇
Hii mada bado ina utata sana kwani sio kwamba ina uhakika kwa asimia kubwa. Hapana nayo ina utata wake kwani Sex ni tendo ambalo mwanadamu mpaka leo anajaribu kujiuliza lengo lake ni nini.
Kwa watu wanaoamini Occult wanaamini kuwa Sex ni gate of eden. Wanaamini kuwa Sex ni muunganiko wa mwanadamu yaani mwanamke na mwanaume. Pia wanaamini Sex ni uumbaji kwani hupelekea uumbaji wa maisha mapya ya mtoto. Occult wamefika mbali kwa kufundisha kuwa Orgasm ni tofauti na sex. Orgasm ni hisia inayopatikana katika sex. WanaOccult wamegawanyika hapa.
* Kuna wanaoamini Sex ndio msingi mkuu
* Kuna wanaoamini Orgasm ndio msingi mkuu na sex sio lazima.
Kwani Orgasm wanaamini inaamsha energy ya kujitambua mwilini.
Lakini mimi baada ya kujifunza sana, nimekuja kukataa kabisa kuwa Sex ni muhimu katika kujitambua. No Sex sio muhimu kwani wanadamu wengi waliokuja kujitambua waliwahi kujitenga na mahusiano na mwanamke kwa kipindi fulani au katika maisha yao yote. Hii ni uthibitisho kuwa sex sio gate to soul bali kuachana na desires ndio gates to soul. Sex ni njia ya kuweka uhai mpya kwa kuleta uhai tena kwenye hali ya uanadamu lakini pia sex ni kifungo ambacho mwanadamu anajifunga ili asijitambue. Ni kama ni njia ya pekee katika kuleta uhai lakini pia ni njia ya kukupoteza pia. Mfano mzuri na wanafunzi wa Yesu waliacha kuendelea na mahusiano na wake zao na kushikilia imani kwa kujitambua. Lengo kuu ni kujitambua kwani unapoishi maisha yasiyo na tamaa, desires, lust na ujinga unaongeza kujitambua na nguvu ya kiimani. Pia sex inapelekea utokwaji wa mbegu za mwanadamu. Wanadamu wengi wanafurahia sex na wanaamini kuwa ni raha lakini hawajui kuwa uwezo wa tone moja la mbegu inayotoka ni sawa na matone 40 ya damu. Kwa maana kuwa mbegu ni aina ya majimaji ya mwili ambayo dhamani kubwa ya uhai imewekwa. Mtu anapotoa mbegu kila saa anapelekea mwili wake kulazimika kujinyima na kutengeneza mbegu kwanza lakini mtu asiyetoa mbegu zake mara kwa mara ile nguvu ya mwili kutengeneza mbegu inapungua na mwili unatengeneza nguvu ya kiroho, kimwili na kiakili. Na hata utafiti wa sasa unasema kuwa mbegu zisipotumika mwili unaziwekeza katika maendeleo mengine ya mwili. Hata ukitaka kujaribu kaa bila sex kwa muda mrefu na siku ukiingia kwenye sex unahisi mchovu na emotional imbalance.
Cha msingi ni kujitambua. Sex sio kitu cha kusema kitumike kuzidisha, na kwa ambao hawana muda na sex au wanadhiri nao wapo sawa kabisa.