sahihisho kidogo"
Siyo jinsia - ni ngono imepewa uzito usiostahili.
Nami kwa kuchangia nitaongezea hivi -
Mtoa hoja, naona unachanganya ngono na mapenzi na huenda ndio over rating yenyewe hii inakoanzia. Unaweza kufanya ngono bila kuwepo mapenzi.Watu huchanganya haya mambo mawili katika kulipa hili tendo uzito usiostahili.Huwa tunasoma au kusikia watu wakisema... afanya mapenzi na mnyama, akamatwa akifanya mapenzi na mtoto mdogo/mchanga ( wakati haya ni matukio ya kihalifu)!
Hata basi pale tendo linapofanywa katika mukhtadha wa ku express mapenzi pia kuna kuongeza chumvi sana katika tendo lenyewe - utasikia watu wakijisifia kupiga mabaoi 10 kwa sekunde nk. Pia kuna kutiliana presha sana katika utendaji.Wanawake hutarajiwa kufanya miujiza ili kuwafurahisha wapenzi wao, na wanaume wenyewe hujitia presha kuhusu ukamilifu wa maumbile yao na kama yatatosheleza wapenzi wao.
The bottomline, kitendo hicho kichukuliwe kama vitendo vingine vya asili alivyopewa binadamu kukidhi kuishi hapa duniani kama kula chakula, kunywa maji, kujikuna unaposikia kuwashwa nk.Sijawahi kusikia watu wakifafanua sana kitendo cha kula na kukipa presha za ajabu zaidi ya kusema chakula kiwe na ladha nzuri, kiandaliwe kwa usafi na salama, kiliwe kwa wakati na mahali muafaka. The same should go for sex!
Ndio mchango wangu mdogo.