Naanza kuhisi kwamba upinzani na JF tunazidi kulalama bila kuchukua hatua. Hivi haiwezekani mtu kufungua mashitaka ili kina Mkapa, Chenge, Yona, Mramba, nk. washitakiwe? Nakasirika sana kuona tukishamaliza kulalama mjadala unafungwa tunahamia kwenye issue nyingine.
Walau kuna matumaini kidogo baada ya wapinzani kupata nuru na kwenda kukagua daftari la mali za viongozi. Je lakini baada ya hapo kuna mkakati wowote wa kuwapeleka mahakamani wakikuta wamedanganya? Au ni hotuba na kusahau jumla wakiahidiwa serikali ya mseto zanzibar? Tuanze sasa jamani kuchukua hatua.