SGR: Dar mpaka Moro na Moro mpaka Dodoma masaa mangapi?

SGR: Dar mpaka Moro na Moro mpaka Dodoma masaa mangapi?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Wakuu mimi nipo Bariadi mitaa ya Gamboshi huku.

Ningependa kujua kwa mlio tumia SGR by experience Dar to Moro na Moro to Dodoma ni masaa mangapi?

Na nauli ni Tsh ngapi ?

Watu wa Mwanza Bariadi Shinyanga na Musoma safari ya kwenda Dar ni mateso huwa tunafika usiku mnene

Napenda kujua ili kuona kama kuna uwezekano wa kutoka kanda ya ziwa saa12 asubuhi kisha unashukia Dom unapanda Treni unaingia Dar

Nataka nifanye tathimini.

Ahsanteni.
 
Wadau mlio panda leo tunaomba majibu please
 
Mkuu ulipanda ya jana ndo mkatumia huo muda. Au ni ule wa kwenye ratiba yao?
Tusubiri majibu maana kwa basi Dar to Moro ni masaa manne moro to Dom masaa matano

Kama huo muda alioutaja ni sahihi basi sitapanda tena mabus
 
Tusubiri majibu maana kwa basi Dar to Moro ni masaa manne moro to Dom masaa matano

Kama huo muda alioutaja ni sahihi basi sitapanda tena mabus
Ukweli ni kuwa safari ya bus Dar to Morogoro au Morogoro to Dar ni saa 5 nzima kwa bus; na kutoka Dar hadi Dodoma au Dodoma hadi Dar kwa bus ni saa 8 nzima. Hiyo ndiyo hali halisi kwa sisi tunaotumia usafiri wa bus.
 
Tusubiri majibu maana kwa basi Dar to Moro ni masaa manne moro to Dom masaa matano

Kama huo muda alioutaja ni sahihi basi sitapanda tena mabus
Nilipanda j4 kutoka Dom tumetoka saa kumi na moja na nusu alfajir tumefika Dar saa mbili na dkk 50 speaking with my own experience
Huu mradi km hawatauhujumu i swear ni mzuri mnooo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakati Dar Dodoma kwa bus ni 29000 naongeza zangu 2000 napanda mwendokasi.
 
Back
Top Bottom