Kuzisifia sio dhambi kwasababu kiuhalisia kabisa huduma zake zinaonekana kuwa nzuri na kurahisisha huduma ya usafiri
Tatizo ninaloliona mimi ni usimamizi mbovu. Nadhani dunia nzima Tanzania ina usimamizi wa kilofa kwenye miradi yake
Wanaoendesha hii miradi hawataki kwenda na mabadiliko ya dunia. Wanang'ang'ania mifumo ya kizamani sana ambayo kimsingi imepitwa na wakati
Nakataa kabisa kwamba serikali haiwezi kufanya biashara. Mimi naamini wanaweza kwasababu wasimamizi wa haya makampuni binafsi yanayofanya biashara ni watu, wamesoma vyuo hivi hivi wanavyosoma watu kama wao walioko kwenye mashirika ya umma, sasa kwanini washindwe?
Kinachowashinda ni kung'ang'ania mifumo ya kizama ambayo kifaa ili kionekane kimeharibika lazima kiache kufanya kazi kabisa halafu kiombewe ukarabati au matengenezo kikiwa hakifanyi kazi na maombi hayo yachukue siku kadhaa bila kujua wanaathiri wateja
Kwa mfano, huwezi kunishawishi mimi eti kwamba upuuzi uliotokea kwenye SGR ni sababu ya mvua ya siku moja tu. Huu ni upuuzi wa juu kabisa
Sent using
Jamii Forums mobile app