SGR inahujumiwa au ni uzembe tu unaotokana na watu kutochukuliwa hatua?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Wanabodi (kwa sauti ya paskali),

Leo tarehe 4 nimefanya uzinduzi wa kupanda treni yetu pendwa ya SGR. Kwa bahati mbaya leo asubuhi kulikua na shida kwenye gridi ya taifa hivyo kujikuta treni karibu zote kuchelewa kwa angalau saa moja, na vyombo vyote vya habari vilitangaza.

Baadae umeme ulirudi na safari kuendelea kama kawaida,ila around mida ya saa 11 jioni safari zikasimama tena kwa zaidi ya masaa manne mpaka muda huu ninapoandika (na tukaendelea kusubiri huenda ikazidi masaa manne).

Tofauti na asubuhi ambapo uma ulitangaziwa kuwa tatizo ilikua umeme kwenye gridi ya taifa,hii ya sasahivi hatujaambiwa ni nini hasa tatizo zaidi ya kuambiwa mafundi wanaendelea kushughulikia tatizo la kiufundi/kimfumo.

Na hata hivyo hakuna chombo chochote cha habari kilichotangaza hadi sasa. Cha kusikitisha ni kuwa hizi SGR hazina huduma ya chakula kama zile treni za zamani,hivyo kila mtu analia njaa hapa (japo mi silii njaa maana najua njaa ya siku moja haiui), ila shida ni kwa watoto ambao zaidi ya zile bites, korosho na chai hakuna kingine kinachouzwa humu.

Najiuliza hivi zile tumbuatumbua zingekuwepo haya mambo yangekua yanajirudia kiasi hiki? Mbona kama hawa jamaa wanakazi kubwa ya kufanya ila wamerelax sana?

Soma Pia: TRC: Treni za SGR zilisimama maeneo matatu tofauti kutokana na hitilafu ya umeme katika Gridi ya Taifa

Na hapo ni mvua ya siku moja tu kwa mikoa ya morogoro na Dodoma, je masika ikikolea kutakua na safari za uhakika kweli?

Nadhani watu wakianza kuwajibishwa akili zitarudi aisee uzembe pia unachangia kwenye hili na tutaishia kulaumu kuhujumiwa na wenye mabasi.
 
Ukiwambia ukaona hawajali
Wambie CDM Wanandamana mitaa hiyohiyo treni ilipokwama watakuwa fasta
 
Hakikaa n huzuni sana pale unaamini umepanda tren ya umeme Ili ukimbizane na mudaa Cha ajabu muda unakuacha ukiwa ktkt ya pori na SGR yakooo..
 
Ni ajabu sana aisee,kwa waliopanda mabasi washafika na wamesahau halafu sisi hatujui saa ngapi safari itarejea. Na hurusiwi kushuka hata ujinyooshe kidogo
 
Mimi nipo Ruvu tangu saa11 jioni hadi muda huu.
 
Ningekuwa mimi, nisingewaachia TRC waendeshe SGR.

Hawana uwezo wala weledi wa kuendesha biashara.

TRC ilihusika na failures zote za reli. Inawezekanaje wao tena na akili zile zile ndogo za scarcity mentality wakafanya tofauti?

Kuna wakati unaona mkusanyiko wa wajinga wengi kwenye seat za mbele, unshangaa
 
Hii nchi kufika tunakotaka si leo wala kesho
 
Ni ajabu sana aisee,kwa waliopanda mabasi washafika na wamesahau halafu sisi hatujui saa ngapi safari itarejea. Na hurusiwi kushuka hata ujinyooshe kidogo
Duuu na kushuka kumbe hakupo 😔😔..polen mkuu ndio nchi yetu ,subiri wanasiasa waje hapo badala ya kuja wataalamu ..
 
Waliruhusu kushuka saizi tunarandaranda huku nje tunacheza na ngedere wa ngelengele
 
Back
Top Bottom