SGR inahujumiwa au ni uzembe tu unaotokana na watu kutochukuliwa hatua?

SGR inahujumiwa au ni uzembe tu unaotokana na watu kutochukuliwa hatua?

Ifike mahala sasa kampuni za serikali ziundwe kwa mfumo wa kuajiri competent professionals waziendeshe.

Hii SGR chini ya hawa TRC tusitegemee maajabu. Sioni akili hizo za kuwezesha hili shirika kufanya biashara na kujiendesha


Muda utasema yote.....
 
Wanabodi (kwa sauti ya paskali),

Leo tarehe 4 nimefanya uzinduzi wa kupanda treni yetu pendwa ya SGR. Kwa bahati mbaya leo asubuhi kulikua na shida kwenye gridi ya taifa hivyo kujikuta treni karibu zote kuchelewa kwa angalau saa moja, na vyombo vyote vya habari vilitangaza.

Baadae umeme ulirudi na safari kuendelea kama kawaida,ila around mida ya saa 11 jioni safari zikasimama tena kwa zaidi ya masaa manne mpaka muda huu ninapoandika (na tukaendelea kusubiri huenda ikazidi masaa manne).

Tofauti na asubuhi ambapo uma ulitangaziwa kuwa tatizo ilikua umeme kwenye gridi ya taifa,hii ya sasahivi hatujaambiwa ni nini hasa tatizo zaidi ya kuambiwa mafundi wanaendelea kushughulikia tatizo la kiufundi/kimfumo.

Na hata hivyo hakuna chombo chochote cha habari kilichotangaza hadi sasa. Cha kusikitisha ni kuwa hizi SGR hazina huduma ya chakula kama zile treni za zamani,hivyo kila mtu analia njaa hapa (japo mi silii njaa maana najua njaa ya siku moja haiui), ila shida ni kwa watoto ambao zaidi ya zile bites, korosho na chai hakuna kingine kinachouzwa humu.

Najiuliza hivi zile tumbuatumbua zingekuwepo haya mambo yangekua yanajirudia kiasi hiki? Mbona kama hawa jamaa wanakazi kubwa ya kufanya ila wamerelax sana?

Soma Pia: TRC: Treni za SGR zilisimama maeneo matatu tofauti kutokana na hitilafu ya umeme katika Gridi ya Taifa

Na hapo ni mvua ya siku moja tu kwa mikoa ya morogoro na Dodoma, je masika ikikolea kutakua na safari za uhakika kweli?

Nadhani watu wakianza kuwajibishwa akili zitarudi aisee uzembe pia unachangia kwenye hili na tutaishia kulaumu kuhujumiwa na wenye mabasi.
"Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, amesema wananchi waondoe hofu kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme katika safari za treni inayotumia umeme akisema treni hiyo ina mkondo wa umeme unaojitegemea.Hayo yalisemwa Februari 26, 2024".
 
Angekuwa Mr Misifa angeruka na watu hapo.

Sometime tunamkumbuka. RIP.
 
Back
Top Bottom