SGR inajengwa juu ya ile ya zamani?

dafity

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2008
Posts
1,858
Reaction score
2,059
Wadau najiuliza hii reli mpya ya kisasa inajengwa kwenye tuta lile la zamani au kuna tuta lake pembeni?

Sijaona picha yoyote ya ujenzi huo naomba aliyenayo atuwekee hapa.
 
Ni tuta lingine jipya kabisa. Nadhani waliamua kuiacha hii reli ya sasa ili iendelee kutoa huduma za usafiri wakati hii mpya ikijengwa. Kumbuka ujenzi wa reli huwa unachukua miaka kadhaa hivyo kuing'oa reli iliyopo sasa ingemaanisha kusimamisha huduma za usafiri wa reli kwa miaka kadhaa na hivyo kuleta kero kwa wasafiri wanaotumia treni. Pia serikali ingekosa mapato kwa muda wote huo. Hilo pato linalotokana na reli ya sasa yawezekena pia linachangia kwenye ujenzi wa hii reli mpya.

Kitu kingine ni kwamba reli ya zamani itabaki ili kusaidia huduma za usafiri kwa ajili ya dharura pale ambapo reli ya kisasa itakapopata tatizo (back up railway). Nadhani hapo umepata mwnaga!
 
Asante kwa majibu mujarabu na yanayoeleweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…