Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa majibu mujarabu na yanayoelewekaNi tuta lingine jipya kabisa. Nadhani waliamua kuiacha hii reli ya sasa ili iendelee kutoa huduma za usafiri wakati hii mpya ikijengwa. Kumbuka ujenzi wa reli huwa unachukua miaka kadhaa hivyo kuing'oa reli iliyopo sasa ingemaanisha kusimamisha huduma za usafiri wa reli kwa miaka kadhaa na hivyo kuleta kero kwa wasafiri wanaotumia treni. Pia serikali ingekosa mapato kwa muda wote huo. Hilo pato linalotokana na reli ya sasa yawezekena pia linachangia kwenye ujenzi wa hii reli mpya.
Kitu kingine ni kwamba reli ya zamani itabaki ili kusaidia huduma za usafiri kwa ajili ya dharura pale ambapo reli ya kisasa itakapopata tatizo (back up railway). Nadhani hapo umepata mwnaga!