SGR Isaka-Mwanza Yafikia Asilimia 44.25

SGR Isaka-Mwanza Yafikia Asilimia 44.25

Hizi barabara zenu sijui huwa wanajenga na nini zichukue mda wote huo.
Kuna masela huko mbali walikua wa3 tu
Mmoja anamwaga kokoto,
2,anasambaza kokoto
3,anamwaga lami na kukandamiza lever.
km1 wameanza nawaona wiki moja washaifuta hiyo kipande,na hapo walikua wanaenda pozi kupiga lunch na kahawa huku wanacheka tu.
Bongo hiyo kl 1 kuijenga ingechukua miaka na hela kibao na isingedumu.
 
..Sgr imegawanywa mapande toka Dar mpaka Mwanza, na Kigoma.

..Na serikali ilieleza kipande cha Dar Moro kitaanza na kufuatiliwa na kipande kingine kuelekea Mwanza na Kigoma.

..Hakuna mantiki ya kujenga kipande cha mwisho wa reli, Isaka kwenda Mwanza, kabla ya kumaliza kipande cha kwanza, na vya katikati.

..Haileti mantiki kuanza ujenzi Isaka Mwanza wakati kipande cha Morogoro to Dodoma / Makutopora hakijaisha. Au Makutopora Tabora Nzega hakijaanza.

Unaweza fikiri hivyo, lakini mwendazake pamoja na madhaifu yake, alikuwa anatumia kichwa kufikiri. Alijua at anytime, he might not be there, kwa hiyo ili ndoto yake ikamilike, lazima atakaye kuwepo asingekubali kipande cha isaka/ mwanza kibaki bila kukamilika
 
Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Isaka mkoani Shinyanga hadi Mkoa wa Mwanza urefu wa kilometa 341 ukijumuisha njia kuu na njia ya kupishana kwenye stesheni unazidi kushika kasi na hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 44.25.

Meneja mradi kipande cha tano cha SGR, Christopher Kalisti alisema wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Alisema kuwa kazi kubwa ya msingi katika mradi huo ni ujenzi wa tuta na kuwa hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 80 wakati mifumo mingine inayofuata juu ya tuta ikiendelea vizuri ikiwemo kutandika reli na kazi hiyo ime-fanywa kwa kilometa 24. Kalisti alisema kuwa wanaendelea kusimika nguzo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme pamoja na kupanda majani kwa ajili ya ulinzi wa matuta.

"Ujenzi wa madaraja kiujumla unaendelea vizuri, tuna mada-raja zaidi ya 600 yanayojumuisha madaraja kwa ajili ya kupitisha mifumo ya umeme, kupitisha mawasiliano, kupitisha wanyama, kupitisha binadamu, kupitisha magari, kupitisha treni ya zamani kiujumla inaendelea vizuri na tumefikia zaidi ya asilimia 60;" alisema.

Naye Waziri wa Uchukuzi, Profesa Mbarawa alisema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo na alitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa kwake kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mdeme alisema kuwa kutokana na mkoa huo kupitiwa na mradi huo wa SGR kama mkoa wamejipanga kuzalisha zaidi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na mifugo.
Mpango ni kuisha lini ? Kabla ya Uchaguzi au baada ya Uchaguzi..
 
Unaweza fikiri hivyo, lakini mwendazake pamoja na madhaifu yake, alikuwa anatumia kichwa kufikiri. Alijua at anytime, he might not be there, kwa hiyo ili ndoto yake ikamilike, lazima atakaye kuwepo asingekubali kipande cha isaka/ mwanza kibaki bila kukamilika

..mradi hauwezi kusimamishwa kwasababu kuna upigaji mkubwa ndani yake.
 
Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Isaka mkoani Shinyanga hadi Mkoa wa Mwanza urefu wa kilometa 341 ukijumuisha njia kuu na njia ya kupishana kwenye stesheni unazidi kushika kasi na hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 44.25.

Meneja mradi kipande cha tano cha SGR, Christopher Kalisti alisema wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Alisema kuwa kazi kubwa ya msingi katika mradi huo ni ujenzi wa tuta na kuwa hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 80 wakati mifumo mingine inayofuata juu ya tuta ikiendelea vizuri ikiwemo kutandika reli na kazi hiyo ime-fanywa kwa kilometa 24. Kalisti alisema kuwa wanaendelea kusimika nguzo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme pamoja na kupanda majani kwa ajili ya ulinzi wa matuta.

"Ujenzi wa madaraja kiujumla unaendelea vizuri, tuna mada-raja zaidi ya 600 yanayojumuisha madaraja kwa ajili ya kupitisha mifumo ya umeme, kupitisha mawasiliano, kupitisha wanyama, kupitisha binadamu, kupitisha magari, kupitisha treni ya zamani kiujumla inaendelea vizuri na tumefikia zaidi ya asilimia 60;" alisema.

Naye Waziri wa Uchukuzi, Profesa Mbarawa alisema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo na alitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa kwake kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mdeme alisema kuwa kutokana na mkoa huo kupitiwa na mradi huo wa SGR kama mkoa wamejipanga kuzalisha zaidi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na mifugo.

Walipe fidia kwa wananchi,
 
Hii ni miradi ya upigaji mtupu.
Ni hadithi tupu.
Mradi gani huo unajengwa milele na bado haukamiliki?
 
mleta mada weka Picha ili Habari yako ikamilike
 
Acha ujuaji wa kijinga, soma vizuri na elewa vizuri bila kukurupuka, na hili ni tatizo kubwa la watanzania wengi wapumbavu.

341km ukijumuisha njia kuu na njia ya kupishana kwenye stesheni, ujenzi wa railway umbali unaesabika mpka zile kilometa 92 za kupishana sio kama barabara.
Analeta ujuaji uchwara anadhani reli ni barabara.
 
Back
Top Bottom