Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,414
- 2,181
1.Wafanyabiashara wa mabasi
Mfano ndugu Ahmed Shabiby aliwahi nukuliwa kwenye mahojiano kwamba basi lake la kwanza alimiliki akiwa na miaka 19. Bila shaka mpaka sasa ana uzoefu mkubwa mno, na ni muda wa kutumia ujuzi huo ku-diversify (kutoweka mayai kapu moja) kumbuka walomtangulia kama Sumry wameswitch kwenye kilimo, Tawakal kwenye mafuta n.k .Je ataunga basi zake zianzie pale abiria wa SGR wanapoishia? Hesabu hizi zinamuhusu Shabiby na Abood ,ni muda wa kukuza vipaji vyao.
2. Wafanyabiashara wa bidhaa
Sokoni hasa matunda, anayewahi kufika sokoni ndo huuza bei kubwa. Amenukuliwa waziri wa uchukuzi Mh.Mbarawa, treni ya mizigo itabeba tani elf kumi ,sawa na malori 500 kwa kila safari moja, hivyo ni muda wa wafanyabiashara wadogo kupanga vyema nini wanunue wapi na wakauze wapi ndani ya muda ili kutengeneza faida kubwa (Super profit)
3. Wasimamizi wa SGR
Ni wazi hii ni treni ya kwanza kwa mwendo kasi. Wasimamizi walinukuliwa wakishukuru ziara yao ya Korea kujifunza kwa vitendo namna ya kusimamia (management) SGR.
Ni muda wa kuonesha vipaji vyao wananchi kuwaona wamejitambua wanasimamia SGR kwa viwango sawa dunia nzima(Universal) au bado wanahisi wako usimamizi wa treni za pole pole (MGR)? Tuwape muda
PIA SOMA
- Majina ya vituo vya tren: Dar Magufuli, Moro Kikwete, Dom Samia, Tabora Mwingi, Shinyanga Karume na Mwanza Nyerere