SGR Itaboresha Vipaji Hivi

SGR Itaboresha Vipaji Hivi

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
1.Wafanyabiashara wa mabasi
Mfano ndugu Ahmed Shabiby aliwahi nukuliwa kwenye mahojiano kwamba basi lake la kwanza alimiliki akiwa na miaka 19. Bila shaka mpaka sasa ana uzoefu mkubwa mno, na ni muda wa kutumia ujuzi huo ku-diversify (kutoweka mayai kapu moja) kumbuka walomtangulia kama Sumry wameswitch kwenye kilimo, Tawakal kwenye mafuta n.k .Je ataunga basi zake zianzie pale abiria wa SGR wanapoishia? Hesabu hizi zinamuhusu Shabiby na Abood ,ni muda wa kukuza vipaji vyao.

2. Wafanyabiashara wa bidhaa
Sokoni hasa matunda, anayewahi kufika sokoni ndo huuza bei kubwa. Amenukuliwa waziri wa uchukuzi Mh.Mbarawa, treni ya mizigo itabeba tani elf kumi ,sawa na malori 500 kwa kila safari moja, hivyo ni muda wa wafanyabiashara wadogo kupanga vyema nini wanunue wapi na wakauze wapi ndani ya muda ili kutengeneza faida kubwa (Super profit)

3. Wasimamizi wa SGR
Ni wazi hii ni treni ya kwanza kwa mwendo kasi. Wasimamizi walinukuliwa wakishukuru ziara yao ya Korea kujifunza kwa vitendo namna ya kusimamia (management) SGR.

Ni muda wa kuonesha vipaji vyao wananchi kuwaona wamejitambua wanasimamia SGR kwa viwango sawa dunia nzima(Universal) au bado wanahisi wako usimamizi wa treni za pole pole (MGR)? Tuwape muda

PIA SOMA

- Majina ya vituo vya tren: Dar Magufuli, Moro Kikwete, Dom Samia, Tabora Mwingi, Shinyanga Karume na Mwanza Nyerere
 
Kwahiyo Mkuu mleta mada unataka kusemaje yaani kuhusu abood na shabiby bado hujasema.. Kwamba una akili ya biashara zaidi yao siyoo!!!
Mkuu huu uchambuzi tuu.Juzi tajiri namba 1 Africa.Alhaji Aliko Dangote pia alikuwa anachambuliwa mradi wake wa kusafisha mafuta ghafi. Mada kuu SGR, yoyote anayeathirika anajadiliwa kwa uzuri.
 
Dr. Zaganza,

..bidhaa zinazoharibika kwa mfano matunda, na mbogamboga, ni rahisi zaidi kuzisafirisha kwa malori toka shambani mpaka sokoni, au kiwandani.

..Sgr inafaa zaidi kusafirisha mitambo, na bidhaa ambazo haziharibiki. Kwa mfano sementi, nondo, mashine kubwa, magari, etc ni baadhi ya bidhaa ambazo zinafaa kusafirishwa kutumia reli.
 
wakati nyie mkisema ndio mwisho wa about na shabiby wenzenu walishawaza namna watanufaika na sgr by being part of it,

tatizo mnakaa vijiweni wenzenu analyse issues na kutega mitego kunufaika na uelekeo wa nchi,
wenye mabasi wameungana wanataka kununua vichwa na mabehewa hivyo watatoa huduma ya train in near future,
 
Dr. Zaganza,

..bidhaa zinazoharibika kwa mfano matunda, na mbogamboga, ni rahisi zaidi kuzisafirisha kwa malori toka shambani mpaka sokoni, au kiwandani.

..Sgr inafaa zaidi kusafirisha mitambo, na bidhaa ambazo haziharibiki. Kwa mfano sementi, nondo, mashine kubwa, magari, etc ni baadhi ya bidhaa ambazo zinafaa kusafirishwa kutumia reli.
Shukrani,nilikuwa silijui hili.
 
Being rich is about vision

Waarabu na wahindi most of them, wapo a head of the time .

Biashara anaisimamisha MTU na sio capital .

Mfano hii SGR ikiwa chini ya usimamizi wa Aboud inaweza kuwa na matokeo chanya kuliko kuwa chini ya serikali.


Vipaji vitaendelea kuwepo.
 
Hao kina Shabiby wanajijali na kutambua biashara zao na wameweka mikakati ya jinsi ya kuendesha biashara zao pengine kabla hata ujenzi wa sgr haujaanza alafu muuza nyapi kama wewe unakuja kujifanya mjuaji kuliko wenye mabasi yao
Sasa mkuu kosa la mleta mada ni lipi mpaka umuite matusi ya viungo vya mwanamke?
 
Back
Top Bottom