SGR na uwekezaji mkubwa wa viwanda Tabora, Dodoma, Singida, Morogoro, Shinyanga

SGR na uwekezaji mkubwa wa viwanda Tabora, Dodoma, Singida, Morogoro, Shinyanga

mwanamichakato

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,090
Napongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika ktk ujenzi wa miundombinu yenye thamani kubwa ktk nchi.

Serikali imetumia zaidi ya Tirioni 8 ktk ujenzi wa SGR..Kilichofanyika ni uwekezaji wa kihistoria ulifanikishwa kwa mapato ya ndani na mikopo ya fedha yenye riba nafuu na isiyo na riba nafuu..

Tuna jukumu la kulipa mikopo na madeni yetu kwa wakati stahiki kuepuka adhabu na malimbikizo kuwa makubwa zaidi..

Ili kufanikisha ulipaji madeni husika lazima tujifunge mikanda haswaa na kuhakikisha uzalishaji na biashara zinashabihiana na mzigo wa madeni tulionayo sasa na baadae..

Treni mpya ya abiria ya kisasa inayofanya kazi ktk miundombinu ya SGR imekuwa gumzo na kivutio kwa watanzania wengi haswa safari za Dar mpaka Dodoma..Mihemuko yetu,Hisia zetu na matamanio hakika yamejaa shauku kubwa..

Nikitafakari kibiashara na ukubwa wa obligations tulizonazo ktk madeni nawiwa kushauri TRC na serikali kwa ujumla kutazama namna ya kufungamanisha maendeleo ya uchumi wa nchi na matumizi yenye tija ya uwekezaji wa SGR.Naamini hatukuwekeza tirions ili tubebe abiria..

Msingi wa uwekezaji ni kufungua collidor kwa kuwezesha usafirishaji wa bidhaa,mazao ya kilimo,Ufugaji,madini kwenda nje ya nchi (Export pia imports kwenda ndani ya nchi (Local Imports) na Transit imports.

Sasa ni wakati wa kupima maeneo ya uwekezaji wa viwanda vikubwa,Mashamba makubwa (Kilimo) kisha vigawiwe bure kwa wawekezaji wa ndani na nje ili kukuza uzalishaji kisha matumizi yenye tija
 
The way we think and conduct our affairs, I don't see major investments from locals. It will the investment by foreigners. Those that see the opportunities and want to make most out of it.

Ukiangalia namna tunavyotafuta na kukusanya kodi, ni wazi hatuna fikra wala nia ya kuhimiza uwekezaji wa wazawa ili kupanua wigo wa makusanyo ya kodi, na kuboresha maisha ya watanzania wa kawaida.
Wazawa wenyewe tuko busy na petty issues. Hatuangalia mapana na marefu ya kuwa sehemu ya nguzo kuu za uchumi.
 
Wizara zote zitengeneze mpango mkakati unaohusisha kwa jinsi gani wanaweza kujenga nchi na kuinua mapato ya serikali kupitia SGR..

Wizara ya Kilimo-Utengaji wa maeneo ya kimkakati ktk kilimo kwa ajili ya export pana zaidi..Mashamba yenye ekari 5000 mpaka 100,000

TAMISEMI-Ufanikishaji wa uwekezaji ktk level ya halmashauri,Tarafa,Kata na Vijiji dhidi ya matumizi ya SGR

Wizara ya Viwanda na Biashara/Uwekezaji-Mnyororo stahiki wa ujenzi wa viwanda vitakavyotumia SGR kusafirisha bidhaa na materials.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa-Uletaji wawekezaji ktk viwanda,Kilimo,Mifugo,etc

Wizara ya Fedha-Mipango na tafiti za kiuchumi ya nini kifanyike kukuza thamani ya fedha,GDP,etc kupitia SGR..

Wizara ya Kazi na Ajira-Ubunifu wa miradi inayofungamana na SGR..

Hivyo taasisi zote zenye mapana ya kuimarisha,Kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi TIC,TPA,EPZA,TANTRADE,TRA,TIRDO,TEMDO,SIDO,TPSF,TCCIA,CTI,etc
 
The way we think and conduct our affairs, I don't see major investments from locals. It will the investment by foreigners. Those that see the opportunities and want to make most out of it...

Nadhani ni issue ya mindset..Hakuna mwekezaji mgeni atatuletea maendeleo kamwe..Lazima tushiriki vema ktk kuondoa umaskini wa watu wetu..Nchi yetu ina utajiri mkubwa mnooo kila kona..Hatupaswi kuwa maskini.

Mfumo wa elimu usifinyangwe kutimiza matakwa ya kisiasa bali maendeleo..Mathalani Shule ya kata kuwa na wahitimu 740 wa kidato cha nne ambapo ktk matokeo 400 wanapata division 4; huku 200 division Zero,100+ devision Three..etc what do you expect?..
 
Kwa nini tuagize vitunguu swaumu toka China/India/Vietnam?

Kwa nini tuagize mafuta ya kula toka Thailand?

Kwa nini tuagize Sukari toka Brazil?

Kwa nini tuagize maharage ya kopo toka nje?

Kwa nini tuagize nyama toka nje? South Afrika..etc

Kwa nini tuagize maziwa ya kopo?

Kwa tuagize samaki wabichi toka China na etc

Kwa nini tuagize nguo na viatu,mabegi?
 
Nadhani ni issue ya mindset..Hakuna mwekezaji mgeni atatuletea maendeleo kamwe..Lazima tushiriki vema ktk kuondoa umaskini wa watu wetu..Nchi yetu ina utajiri mkubwa mnooo kila kona...

Kuna wakati najiuliza kwanini tunaendesha mambo yetu kama vile hakuna kesho? Tuna soma na kuelimika kweli?
 
Napongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika ktk ujenzi wa miundombinu yenye thamani kubwa ktk nchi...
Msingi wa uwekezaji huu ni maendeleo kwa taifa (wananchi na bila kumung'unya maneno, watanzania waafrika).
Ni lazima kuwa makini na uwekezaji kutoka nje, kwani taifa laweza kuwa watumwa katika ardhi yake.

Kodi isitumike kuwanufaisha wageni.

Fikra za ukombozi ziendelezwe kuelekea kwenye uchumi kwa kuwa kisiasa tulishavuka.
 
Napongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika ktk ujenzi wa miundombinu yenye thamani kubwa ktk nchi.

Serikali imetumia zaidi ya Tirioni 8 ktk ujenzi wa SGR..Kilichofanyika ni uwekezaji wa kihistoria ulifanikishwa kwa mapato ya ndani na mikopo ya fedha yenye riba nafuu na isiyo na riba nafuu...
Hakuna haja ya kupima upya namna ya kuwekeza viwanda; wao wafuate plani alizoasisi Nyerere tu mradi waziboreshe kuendana na wakati tu. Kama hawazijui au hawazikumbuki, mimi nitawajulisha.
 
Hakuna haja ya kupima upya namna ya kuwekeza viwanda; wao wafuate plani alizoasisi Nyerere tu mradi waziboreshe kuendana na wakati tu. Kama hawazijui au hawazikumbuki, mimi nitawajulisha.

Umenena Vema

Masterplan ya viwanda chini ya uongozi wa Mwl Nyerere ilikuwa na maono makubwa mnoo.

Hujuma za Walanguzi na wachuuzi vikaua viwanda lukuki kwa faida binafsi

Tunalo la kujifunza.
 
Kuna wakati najiuliza kwanini tunaendesha mambo yetu kama vile hakuna kesho? Tuna soma na kuelimika kweli?

Tujenge uchumi imara ktk mikoa ya pembezoni mwa nchi..Mipango na mikakati ya makusudi lazima ibuniwe na kutekelezwa..Natambua Serikali imeanza kufanya kwa kiwango fulani..INAWEZEKANA KUFANYA ZAIDI

Kufanyike mikakati ya makusudi ya kuzuia vijana kujazana mijini ktk vibarua vyenye kusimika umaskini kwa kaya..Bodaboda na betting si ajira endelevu za kujenga taifa..
 
Kwa nini tuagize vitunguu swaumu toka China/India/Vietnam?

Kwa nini tuagize mafuta ya kula toka Thailand?

Kwa nini tuagize Sukari toka Brazil?

Kwa nini tuagize maharage ya kopo toka nje?

Kwa nini tuagize nyama toka nje? South Afrika..etc

Kwa nini tuagize maziwa ya kopo?

Kwa tuagize samaki wabichi toka China na etc

Kwa nini tuagize nguo na viatu,mabegi?
Tunaagiza kwa sababu watanzania kwa asili hawapendi kazi na hawapendi kujitumia na wala hawajihangaishi kutafuta fursa. Hizo sekta zote ulizotaja Watanzania wanafanya kazi kimazoea na wanaridhika mapema sana hivyo uzalishaji unakuwa chini ukilinganisha na mahitaji ya soko.

Hadi dunia ya leo wanafuga kwa kuangalia idadi ya mifugo bila kuianzia ubora na hawataki kufuga mifugo michache yenye ubora wa soko.

Ukija kwenye mazao bado tunalima kijadi kabisa. kijishamba kila kina aina ya mazao hadi unashindwa kujua huyu mtu analima zao lipi hasa. Hongera kwa akulima wa Mpunga angalau uzalishaji umepanda ingawa nako tija ni ndogo kutokana na matumizi ya pembejeo yasiyokidhi viwango na matumizi mabaya ya viauatilifu na mbolea.

Hii nchi changamoto inaanzia kwa wananchi wake.
 
Usemalo lina ukweli?

It begins with us

Je nini kinatuzuia wasomi na wenye exposure kufanya kilimo cha kisasa?

Nini kinatuzuia wasomi na wenye exposure kushiriki siasa shindani na kuchechua siasa za nchi kwa kushiriki kwenye michakato ya kisera na mipango kwa maendeleo thabiti?..

Tuchukue hatua na kuwa mfano kwa wengi..Tunaweza
 
Soma vizuri mwisho wa andishi langu. Nimesema changamoto za Tanzania ni Watanzania wenyewe. Acha umaskini utupige KWANZA hadi tukae mguu sawa.
 
Tumepteza fedha bure tu kujenga SGR. Jiwe alikuwa mkurupukaji sana kwasabb ya ushamba wake. Tunajenga SGR ili watu wawahi wapi? Kufanya nn?
(Tangu izinduliwe tumepata faida gani? Sana sana naanza kusikia vilio vya wahuni kupanda bure).

Baada ya kujenga ndipo tunaanza kufikirika matumizi yake? Ujinga mkubwa huu. Tulipaswa kuwa na matumizi ya reli hii ndipo tuijenge.
 
Duh we noma kweli, Kwa upande wangu hakuna tulichopoteza Usafirshaji na uzalishaji ni vitu vinavyotegemeana, kimojawapo kinaweza kuwa factor ya kumuamsha mwenzie, tujipe mda maana umeme wa uhakika tunao na Tumepata means nyingine ya usafirishaji, Tudeal sasa na mapungufu mengine yaliyobaki na kwenye hili viongozi wetu wanapaswa kupambana haswa
 
Bahati Mbaya hatunae tena, lakini ni wazi alipanga ndio maana Bandari iongezwa kina, bwawa la umeme likajengwa na SGR ikajengwa, suala la uzalishaji viwandani na kwenye kilimo ni suala letu Mimi na wewe .
 
Hakuna haja ya kupima upya namna ya kuwekeza viwanda; wao wafuate plani alizoasisi Nyerere tu mradi waziboreshe kuendana na wakati tu. Kama hawazijui au hawazikumbuki, mimi nitawajulisha.
Kama hata theluthi moja ya mipango ile inge fanikiwa, nchi hii ingekuwa mbali sana wakati huu.
 
Duh we noma kweli, Kwa upande wangu hakuna tulichopoteza Usafirshaji na uzalishaji ni vitu vinavyotegemeana, kimojawapo kinaweza kuwa factor ya kumuamsha mwenzie, tujipe mda maana umeme wa uhakika tunao na Tumepata means nyingine ya usafirishaji, Tudeal sasa na mapungufu mengine yaliyobaki na kwenye hili viongozi wetu wanapaswa kupambana haswa
Nina hofu kubwa sana na reli hiyo.
Pengine ni kwa kutojuwa yanayo fanyika ndani kwa ndani na mipango ya uendeshaji wa reli yenyewe. Sina taarifa za kunipa matumaini makubwa kwamba maandalizi ya uendeshaji wa reli hiyo yamefanyika ipasavyo na hakutakuwa na matatizo yale yale tuliyo kumbana nayo miaka yote. Tukitazama mfano wa BRT..., . Hivi kutakuwepo na tofauti kubwa kati ya reli hii na huu mpango wa mjini tu hapo Dar?

Mfano wa reli iliyo jengwa na wachina, hapo jirani yetu. Uendeshaji wa reli hiyo umesimamiwa hadi sasa na wachina wenyewe, na ndio wanaowafundisha wenyeji kuendesha mradi huo wakati mkataba wao utakapo kwisha.
Wenyeji sasa wamefuzu na wanashikiria karibu nafasi zaidi ya asili mia 90 kwa sasa, na uendeshaji unakwenda vizuri.
Sisi huu wa kwetu, sijasikia kama watu wetu wamekwenda mafunzo katika uendeshaji wa reli hiyo. Sijui, kwa sababu naona mambo mengi kwetu ni kama siri ya wenyewe.
 
suala la uzalishaji viwandani na kwenye kilimo ni suala letu Mimi na wewe
Nakubaliana na kauli hii, lakini pamoja na kuwa swala kuwa letu, serikali haiwezi kamwe kujiondoa katika hatua hiyo ili kufanikisha hizo shughuli za wananchi, kwa mfano ruzuku ya mbolea na maswala mengi mengine katika shughuli hizo.
 
Back
Top Bottom