SGR ya Kenya yaendelea kuifilisi nchi, Sera za uchumi wa kibepari zalaumiwa.

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

SGR ya Kenya pamoja na kwamba imeanza kutengeneza hasara kutokana na gharama kubwa zilizotumika kwa kipande cha Mombasa Nairobi kuwa ghali sana, bado serikali ya Kenya imeshindwa kuzuia wezi na rushwa katika mradi huo jambo ambalo linasababisha ujenzi wa kipande cha Nairobi hadi Naivasha kuwa ghali zaidi ya Mombasa Nairobi.

Sababu kubwa inayotajwa ni gharama kubwa za kulipa fidia ya ardhi ukilinganisha na Tanzania. Wasomi na wnaharakati Mbalimbali wameonyesha kutamani mfumo wa Tanzania wa kumiliki ardhi na kuonya kwamba, SGR ya Kenya haitoweza kushindana na ile ya Tanzania kutokana na gharama kubwa inayotumika Kenya.

Kitu kinachosikitisha ni kuona kwamba, makosa yaliyojitokeza katika ujenzi wa kipande cha Mombasa - Nairobi, bado yameendelea kujitokeza katika kipande cha Nairobi - Naivasha, bila kurekebishwa, huenda hilo pia likawa ni sababu moja wapo kwa China kukataa kutoa fedha zaidi baada ya kuona usimamizi dhahifu wa serikali ya Kenya.
 
off topic:
najaribu tu kuwaza endapo ile jana harambee stars wangemfunga algeria, sijui sisi watanzania "tungeambia nini watu hapa jf na kule twitter".

by the they sitaki kuwa mnafiki, nilifarijika sana kwa algeria kuifunga kenya. sisi ni "dugu" ya baba moja.
 
Huu mradi ni finance+manage+reap enough bigger money times 30 of your capital + commission when tired and dilapidated

Sasa kwenye mfumo kama huu ambao unaweza kuwa sustained kwenye banana Republic tu chini ya wachina ni vipi unaamini report zao za mapato

Hiki ndio kile kilikua kwenye bandari ya Bagamoyo yaani wenyewe ndio wapo kwenye board of directors, hakuna mkenya humo ndani, wao wanaletewa tu mahesabu leo ni hasara tupu at the same time wachina wanachota pesa hatari, mishahara yao tu wanaojilipa hata uhuru haoni ndani.
 
Gutter Press
Nyinyi hamuwajui wachina, yaani watawatafuna weee baada ya miaka 15 mkileta zogo wanafinance kipande cha SGR mpaka Nyanza then wanaendelea kuwatafuna kama miaka 5 hivi then mkileta kelele wanafinance tena kipande kingine mpaka Malaba, mambo yatakua hivyo mpaka wamalize Kenya yote hapo ni miaka 50 iyajo wenyewe wakiwa ndio top management ya project nzima

Kuna wachina watastaafia kwenye hii SGR yenu na kulipwa pensions kwa pesa za SGR.
 
Yaani ndoa ya mkeka ,aliyeoa wanamjua na aliyeolewa wanamjua
 
Ilinibidi nicheke na Kunywa Juice kwa raha na nikasahau maumivu Yote
Akicheza Uganda navaa jezi ya Uganda mwanzo mwisho
lakini hii minyanga'au Never
 
duuu, sasa hawakujifunza na ile iliyotokea Mombasa Nairobi?
Hilo si jambo jema kwa majirani, wajipange.
Pia tatizo si mfumo wa kumiliki ardhi, bali ni rushwa. wanalipana fidia kubwa kuliko bei ya soko la ardhi.
 
Sio wewe...ni hyo insha tu...utakufa kw presha
 
Jamani[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Serekali ilikua inataka kuwalipa hawa jamaa wa phase 2A SGR between KSH 10-20 million ($100k-$200k) kulingana na majengo/maendeleo yalio juu ya hio ardhi ambayo SGR itapitia ...



Jamaa wengine kama huyu hapa Chini wakaenda kotini kuzulia serekali wakisema maisha Yao yote yako hapo na tangu wanunue hio ardhi na kuendeleza Hilo eneo, thamani ya hio ardhi imeongezeka mara dufu au hata zaidi na pia uchungu wa kuhamishwa ni mkubwa kwahivyo wanataka wapewe fidia ya $1 million USD (100 million ksh) kila mtu alie na nyumba nzuri .. hapo nakubali wame exergirate!



Hizo kesi zimekua zikichelewesha phase2A kukamilika hata baada ya serekali kuwapatia final offer ya atleast ksh 25million per houshold, sasa serekali imeshindwa ku negotiate zaidi ya hapo manake gharama ya fidia itakua kubwa mno, imeamua kutumia kipengee cha Sheria kinacho ruhusu "compulsory acquisition of land for national development" hata kesi ikiwa inaendelea mahakamani, mtu akikubali anapewa 25m yake, akikataa anaendelea kungoja kesi ikamilike na koti iamue fidia halisi.





Huu mfuko wetu wa 'kipebari' Una changamoto tele lakini nitaukumbatia kila mara kuliko mfumo kama huo wenu ambapo ardhi yote ni ya serekali na serekali ikiamua basi hakuna mtu ana nguvu yoyote .... Kwa huu mfano wa SGR, serekali mara ya Kwanza ilikua imepanga kulipa maximum 15m, lakini baada ya negotiation ikapandisha Hadi 25m, wenye manyumba nao wakakataa hio hela na kuitisha ya juu kabisa 100m ambayo ni too much lakini kesi iko mahakamani baada ya kutofikiana makubaliano, sasa mahakama kama arbiter itafanya independent survey /estimation kulingana na thamani halisi ya hio ardhi na chochote kitalichojengwa juu yake... Huu ndo mfumo tuliouchagua, hakuna mtu ata dhulumu au kudhumiwa na serekali....





Hebu fikiria iwe ni wewe ilinunua robo ekari Kwa shiling 4 million na kujenga nyumba hii na 10million alafu miaka kumi baadae serekali ije ivunje hio nyumba na ikupatie 15 million pekee! Sahii bei ya ardhi kama hio ni 8 million kwahivyo hautakua na uwezo wa kununua ardhi nyengine na ujenge nyumba nyengine kama hio na 15m kwahivyo lazima utaitisha fidia kubwa zaidi .. lakini unapoitisha fidia kupita kiasi, serekali nayo inaweza kukataa na nyote mkaenda mahakamani.





Compulsory acquisition, hawa jamaa watalipwa kesi yao ikiamuliwa kortini ujenzi wa SGR umekua hauwezi enzelea
eneo Hilo la mgong tangu 2017, SGR phase2A inafaa iwe imekamilika mwezi huu wa Juni lakini imebidi isongeshwe hadi September kwasababu ya hawa jamaa, lakini kwa upande mwengine naelewa kama ingekua ni nyumba yangu ningeipigania na nguvu zangu zote hata kujifunga na sururu na kufuli Kwa mlango wa nyumba na nimeze funguo na spare!!!!!!!







 
Usimtukane mkunga_uzazi ungalipo, usitukane mamba kabla ya kuvuka mto
 
Mahakama ndio inafanya valuing, kwani ninyi hamna mthamini mkuu wa serikali {General Assessor or Appraiser} afanye hiyo kazi? Au ndio miamya ile ile ya wizi?

Huu ubepari una make sense kwenye mataifa yaliyoendelea sasa Hapo mwananchi mlalahoi, serikali nayo lalahoi taabu na nusu, mnaifilisi serikali yenu kwa kutaka pesa mingi wakati yenyewe ilishafilisika, hizo pesa itabidi ikakope kwa business rates loans kutoka Beijing.
 
kwani serikali haina mthamini majengo????
 
Tatizo lako wewe unapenda kutoa vitu kichwani mwako ili kuhalalisha wizi na rushwa viendelee huko kwenu. Ukisikiliza vizuri hao " penalists", wanazungumza tofauti na wewe, sasa wewe unajua zaidi, au una akili nyingi kuliko hao wote?, karibu wote wanasema malipo yanavyofanyika yametawaliwa na rushwa, kwamba hao hao viongozi Serikalini ndio wabaohusika kupandisha bei ya ardhi au nyumba. Wao wanasema wazi kwamba watu wanaodai 25M, thamani halisi ni 2M.

Acha kudanganya watu, NYUMBA zenye thamani ya Kshs 25M hazifiki hata 2%, hiyo NYUMBA uliyoweka katika picha, thamani yake sio zaidi ya Kshs 15M, tatizo lenu mnapenda sana kukuza mambo ili mpate pesa nyingi, matokeo yake serikali yenu inafilisika.
 
Hahahaha , kumbe wazimu wewe! Eti millioni mbili!!!! Mimi natoka pwani na hata huko ploti karibu na eneo lilioendelea hauipati hata Kwa millioni tano! Labda uingie kichakani Kwa waliorithi ardhi ya mababu zao ndo watakuuzia Kwa bei ya Chini lakini mtashare title deed ya shamba .
Eneo ninaloishi hapa Nairobi, jirani yangu ameuza ekari moja Jan mwaka huu kwa 24 million! Yani empty field ilikua ni nyasi Tu ndo ziko eneo hilo!

Sometimes kama haujui kitu afadhali unyamaze, nipatie mkenya mmoja hapa ambae atasema hio nyumba ni worth 2 million!!!!! Unasikiza hotuba za watu wa mtaani ambao hawamiliki chochote! That house + land Kwa soko la leo si chini ya millioni 15 ksh, you can take that to the bank!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…