Serekali ilikua inataka kuwalipa hawa jamaa wa phase 2A SGR between KSH 10-20 million ($100k-$200k) kulingana na majengo/maendeleo yalio juu ya hio ardhi ambayo SGR itapitia ...
Jamaa wengine kama huyu hapa Chini wakaenda kotini kuzulia serekali wakisema maisha Yao yote yako hapo na tangu wanunue hio ardhi na kuendeleza Hilo eneo, thamani ya hio ardhi imeongezeka mara dufu au hata zaidi na pia uchungu wa kuhamishwa ni mkubwa kwahivyo wanataka wapewe fidia ya $1 million USD (100 million ksh) kila mtu alie na nyumba nzuri .. hapo nakubali wame exergirate!
Hizo kesi zimekua zikichelewesha phase2A kukamilika hata baada ya serekali kuwapatia final offer ya atleast ksh 25million per houshold, sasa serekali imeshindwa ku negotiate zaidi ya hapo manake gharama ya fidia itakua kubwa mno, imeamua kutumia kipengee cha Sheria kinacho ruhusu "compulsory acquisition of land for national development" hata kesi ikiwa inaendelea mahakamani, mtu akikubali anapewa 25m yake, akikataa anaendelea kungoja kesi ikamilike na koti iamue fidia halisi.
Huu mfuko wetu wa 'kipebari' Una changamoto tele lakini nitaukumbatia kila mara kuliko mfumo kama huo wenu ambapo ardhi yote ni ya serekali na serekali ikiamua basi hakuna mtu ana nguvu yoyote .... Kwa huu mfano wa SGR, serekali mara ya Kwanza ilikua imepanga kulipa maximum 15m, lakini baada ya negotiation ikapandisha Hadi 25m, wenye manyumba nao wakakataa hio hela na kuitisha ya juu kabisa 100m ambayo ni too much lakini kesi iko mahakamani baada ya kutofikiana makubaliano, sasa mahakama kama arbiter itafanya independent survey /estimation kulingana na thamani halisi ya hio ardhi na chochote kitalichojengwa juu yake... Huu ndo mfumo tuliouchagua, hakuna mtu ata dhulumu au kudhumiwa na serekali....
Hebu fikiria iwe ni wewe ilinunua robo ekari Kwa shiling 4 million na kujenga nyumba hii na 10million alafu miaka kumi baadae serekali ije ivunje hio nyumba na ikupatie 15 million pekee! Sahii bei ya ardhi kama hio ni 8 million kwahivyo hautakua na uwezo wa kununua ardhi nyengine na ujenge nyumba nyengine kama hio na 15m kwahivyo lazima utaitisha fidia kubwa zaidi .. lakini unapoitisha fidia kupita kiasi, serekali nayo inaweza kukataa na nyote mkaenda mahakamani.
Compulsory acquisition, hawa jamaa watalipwa kesi yao ikiamuliwa kortini ujenzi wa SGR umekua hauwezi enzelea
eneo Hilo la mgong tangu 2017, SGR phase2A inafaa iwe imekamilika mwezi huu wa Juni lakini imebidi isongeshwe hadi September kwasababu ya hawa jamaa, lakini kwa upande mwengine naelewa kama ingekua ni nyumba yangu ningeipigania na nguvu zangu zote hata kujifunga na sururu na kufuli Kwa mlango wa nyumba na nimeze funguo na spare!!!!!!!