SGR yetu waweke Polisi au JKT chooni!

SGR yetu waweke Polisi au JKT chooni!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Huu ni ushauri wangu tu kwa kuanzia kila choo kiwe na askari mlangoni kukagua kila anayetoka chooni kama kachafua au kakiacha choo kisafi kama alivyokikuta.

Na atakayechafua aidha asafishe mwenyewe au apigwe faini ndefu.

Bila ya hivyo itakuwa SGR ya kichocho na kipindu pindu baada ya safari ya kwanza tu, I know my people …
 
Hata hivo hizo ndo kazi za polisi wetu. Sioni ajabu.

Tuje tuwaombee mechi ya kirafiki hata na Afghanistan...
 
huu ni ushauri wangu tu kwa kuanzia kila choo kiwe na askari mlangoni kukagua kila anayetoka chooni kama kachafua au kakiacha choo kisafi kama alivyokikuta.
na atakayechafua aidha asafishe mwenyewe au apigwe faini ndefu.

billa ya hivyo itakuwa sgr ya kichocho na kipindu pindu baada ya safari ya kwanza tu, I know my people …
Inabidi wafanye hivyo tu, hakuna namna.
 
huu ni ushauri wangu tu kwa kuanzia kila choo kiwe na askari mlangoni kukagua kila anayetoka chooni kama kachafua au kakiacha choo kisafi kama alivyokikuta.
na atakayechafua aidha asafishe mwenyewe au apigwe faini ndefu.

billa ya hivyo itakuwa sgr ya kichocho na kipindu pindu baada ya safari ya kwanza tu, I know my people …
hakuna haja ya polisi, education tu inatosha. polepole watu watakuwa wastaarabu na kujiendesha wenyewe. hana maisha ya kawaida, awareness ya kutotupa takataka ikifanyika kwa muda fulani raia wenyewe watachungana. nimependa mabasi ya kisasa yenye choo, kabla hamjaondoka wanatangaza kabisa, kwamba choo hii ni kwaajili ya haja ndogo tu, marufuku haja kubwa; na hakuna anayefanya haja kubwa. na tren watangaze tu kwamba hakikisha unatumia choo vizuri na kwa usafi kama huwezi sema usaidiwe kwa maelekezo. by time watu watacope na tabia ya ustaarabu itazoeleka. ukitaka kitu kifanikiwe wacha raia wawe ndio walinzi kuliko polisi.

hata hivyo, labda kwa ajili ya ulinzi wa ndani na kwenye stesheni, kuna vijana wetu wengi wamepita JKT hawana ajira, kabla hawajajiingiza kwenye shughuli mbaya wapewe ajira hao,wawekewe kipaumbele kwaza kwasababu hilo linaendana na yale waliyosomea.
 
huu ni ushauri wangu tu kwa kuanzia kila choo kiwe na askari mlangoni kukagua kila anayetoka chooni kama kachafua au kakiacha choo kisafi kama alivyokikuta.
na atakayechafua aidha asafishe mwenyewe au apigwe faini ndefu.

billa ya hivyo itakuwa sgr ya kichocho na kipindu pindu baada ya safari ya kwanza tu, I know my people …
Kwanini wawekwe askari ? Unawekaji watu ambao makazi yao tu waliyowekwa sio nadhifu atawezaje simamia usafi?hebu tuwe serious kidogo na mambo ya msingi kushindwa ku maintain usafi ni namna fulani yakuonesha umaskini na ujinga tulionao
 
Waweke tu vyoo vya sensa mkuu vinavyojisafisha mtu akimaliza haja zake.
 
Mi nadhani TRC ihakikishe wanaopanda wasiwe wasukuma au waha wapande treni ya zamani ili kulinda usafi.
 
Chooni ni sehemu privacy hakuna Sheria ya namna hiyo duniani kote na haitakuja kutokea chooni kukawa na camera
Kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa.Huulizwi umefanya nini.Ukitoka tu kuna mtu mlangoni anakusubiri asafishe tena mara nyengine wa jinsia tofauti.
Halafu kwa ujumla mtu akiingia chooni inategemea alikuwa na hali gani na alikwenda kufanya nini.Wakati mwengine unatamani uwache choo kisafi lakini hali hairuhsusu inabidi utoke tu.
Kama maji ya kutosha hakuna utafanyaje.
 
Back
Top Bottom