Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
SGT MWAJABU BEST LADY AGAINST VIOLENCE TANZANIA AKABIDHI TUZO KWA RPC KILIMANJARO
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Simon Maigwa amepokea tuzo mbili alizotunukiwa SGT Mwajabu Mzee wa Kitengo cha Dawati Jinsia na Watoto Mkoa wa Kilimanjaro alizoshinda Julay 18 mwaka huu Mkoa Morogoro kutoka Shirika la Ladies Talk Tanzania.
SGT Mwajabu alikabidhi tuzo hizo Agosti 7, 2026 pamoja na cheti cha Pongezi alichotunukiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura baada ya kupata ushindi huo wa tuzo mbili Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Kamanda Maigwa alimpongeza SGT Mwajabu kwa jitihada kubwa za kupinga ukatili katika Jamii jambo ambalo limeheshimisha Jeshi la Polisi na Wananchi wa Kilimanjaro.
Kwa upande wake SGT Mwajabu alisema anamshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania na Kamanda Maigwa kwa malezi mazuri yanayomfanya kupata nguvu ya kufanya kazi kwa misingi ya haki, weledi na nidhamu ya hali ya juu.
Sgt Mwajabu aliibuka mshindi wa tuzo ya "The best Lady in violence against human and Children" na tuzo ya "Overall Winner of Ladies Talk Tanzania" zilizoshindaniwa kwa kupigiwa kura mtandaoni kote nchini zikiwa na washiriki zaidi ya 48.