Amoeba youv said it,sio lazima iwe buku tano halisi nadhani yeye ametumia hiyo kama mfano tu kwa yule ambaye anacho kiasi kidogo kwa kuanzia na sio wale wenzio wanaosemaga ana mil 100 afanye biashara gani?(who knows km kweli anayo mill mia kweli au ni maneno tu?) sasa hali halisi ya kibongo tunaifahamu tulio wengi tusikariri kisa kasema mill 100 ukapiga hesabu ya 100 chukua idea weka kwenye biashara/mazingira yako halafu uone.
Kuna mambo mnashindwa kuelewana, "wewe" hiyo elfu tano huwezi kufanyia biashara, kwa mtu anayeanzia chini huo ni mtaji tosha kwake. Kumbuka kwamba, hiyo mil50 ambayo wewe unaona inatosha kuanza biashara kuna mtu ukimpa hiyo pesa anaona unacheza, ni pesa ndogo sana kwa level yake na hataona biashara ya kuifanyia zaidi ya kula!
Amoeba
refer to my phrase "lets be realistic"
tuachane na nadharia hatutafika mbali, kila siku watanzania wanalia kuhusu mitaji halafu leo hii tunasupport kwamba TZS 5,000 inaweza kufanya biashara ? swali la msingi ni je unaweza ku "break even" ?
Mods pelekeni jokes huu uzi
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo
Sasa hapa AMOEBA ndiyo umeliweka hili suala vizuri, hasa baada ya kusema kama mwingine hawezi kuanzisha biashara kwa hicho kiasi, yupo anayeweza. Lakini ni vyema tukikumbuka kwamba huyo mtu anayezungumziwa kwenye post ni Graduate (ingawa hajasema ni degree au certificate), yeye anasema "kumbuka hapo ndio numemaliza chuo" kwa huo msisitizo ni wangu.
Infact hatusemi kwamba hiyo amount (Tsh.5000) haiwezi kuanza biashara, (kwani wauza karanga wanaanza na mtaji gani?) bali ni lazima uchanganye na advantage ya mazingira mtu aliyopo (ambayo kwa bahati mbaya wengi wanashindwa kuyaequate na fedha). Lakini kwa hawa graduate wetu!... (mimi nawaweka hapo kwenye blue)
Hata elfu tano ya jirani zetu kenya bado utakaa sana,labda iwe elfu tano ya wamarekani ndio mambo yatakua safi.
halafu huyu jamaa anataka kukwepa kulipa kodi, biashara gani hii?
Watu wengi ni maskini, si kwa sababu hakuna biashara, LA HASHA, kwa sababu ya kukosa MAWAZO, UTHUBUTU na visingizio kama unavyotoa.
Watu wengi waliofanikiwa kwa kutegemea mitaji ya pesa midogo, ukumbuke wana mitaji mingine. Naona kuna umuhimu wa kufundishana maana ya mtaji.
Ukiwaeleza watu mtaji, wengi wanafikiria kwa kipesa peke yake, aah Sh. 5,000 tu itamtoa kivipi. Wanasahau, kuangalia ndani ya mtu. Ndani ya mtu , kumejaa mtaji mkubwa, Ok tuwe wahalisia hapa kwa kutaja vitu ambavyo ni mtaji.
1.Mtu mwenye ya dhati kufanikiwa katika biashara yake - Huo ni mtaji
2. Wazo - La biashara yako, namna ya kuanza, kukua na kupanuka - mtaji mwingine
3.Mazingira - Hapa Tz tunao uhuru wa kufanya biashara maeneo mengi tu bila vikwazo ,ikiwemo malipo
4. Watu - Idadi ya watu unaowajua kwenye eneo lako, ambao wanaweza kuwa wateja wako wa kwanza na hata kukusaidia kimawazo.
4. Uwezo wa kutokata tamaa na kujilinganisha na wengine isivyofaa-
5. Afya njema
Ukiangalia kuna mambo mengi yanaweza kuwa sehemu ya mtaji na kukuunga mkono. Lakini dunia na hasa Tanzania , imejaa.
a) Wakosoaji- aah mtu wa chuo kikuu aanze na sh. 5,000
b) Wakatisha tamaa- huwezi kufanikiwa kwa mtaji mdogo
c) Tanzania imejaa ufisadi, unafikiri watu wanafanikiwa bila ufisadi
d) Waangaliaji tu na kuahirisha kila jambo.
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo
leo nimeelewa almost 90% ya watanzania hawana uelewa wa mtaji wa biashara na biashara na ujasiriamali kwa ujumla.... tunahitaji kujielewa our inner selves ndio itakuwa rahisi kuelewa ujasiriamali na uthubutu wa kufanya chochote popote na kwa gharama yoyote no matter how little/small or big it takes..NIA YA DHATI na UJASIRI wa kuamini kuwa UNAWEZA hii ni silaha tosha ya mafanikio...
swali la kizushi...wakati dunia haina/ haitumii pesa kama means of exchange watu walikuwa hawafanyi biashara?... mtaji ulikuwa ni nini?...gold, diamond, slaves, mazao, mifugo etc.....TUJIONGEZEEE WATANZANIA TUKITHUBUTU TUNAWEZAAAA.
Unajua ndo maana nilisema hapo awali kuwa mie hapo ni kula kulala. kwa hiyo baadhi ya vianzio nadesa home hapo mkuu