Watu wengi ni maskini, si kwa sababu hakuna biashara, LA HASHA, kwa sababu ya kukosa MAWAZO, UTHUBUTU na visingizio kama unavyotoa.
Watu wengi waliofanikiwa kwa kutegemea mitaji ya pesa midogo, ukumbuke wana mitaji mingine. Naona kuna umuhimu wa kufundishana maana ya mtaji.
Ukiwaeleza watu mtaji, wengi wanafikiria kwa kipesa peke yake, aah Sh. 5,000 tu itamtoa kivipi. Wanasahau, kuangalia ndani ya mtu. Ndani ya mtu , kumejaa mtaji mkubwa, Ok tuwe wahalisia hapa kwa kutaja vitu ambavyo ni mtaji.
1.Mtu mwenye ya dhati kufanikiwa katika biashara yake - Huo ni mtaji
2. Wazo - La biashara yako, namna ya kuanza, kukua na kupanuka - mtaji mwingine
3.Mazingira - Hapa Tz tunao uhuru wa kufanya biashara maeneo mengi tu bila vikwazo ,ikiwemo malipo
4. Watu - Idadi ya watu unaowajua kwenye eneo lako, ambao wanaweza kuwa wateja wako wa kwanza na hata kukusaidia kimawazo.
4. Uwezo wa kutokata tamaa na kujilinganisha na wengine isivyofaa-
5. Afya njema
Ukiangalia kuna mambo mengi yanaweza kuwa sehemu ya mtaji na kukuunga mkono. Lakini dunia na hasa Tanzania , imejaa.
a) Wakosoaji- aah mtu wa chuo kikuu aanze na sh. 5,000
b) Wakatisha tamaa- huwezi kufanikiwa kwa mtaji mdogo
c) Tanzania imejaa ufisadi, unafikiri watu wanafanikiwa bila ufisadi
d) Waangaliaji tu na kuahirisha kila jambo.