Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!


Lakini hata kilimo kinategemea usindikaji pia. Hao wasindika matunda (kama NDYOKO) ni important stakeholder in the value chain
 
Sasa jamani si mwendo wa polepole hiyo elfu nne au tatu ya faida kwa siku mara mwezi ni kama 100,000. Akitunza na kupanua biashara yake baada ya miezi 3 basi anapata wastani wa 300,000 hii inakuwezesha kufanya kitu kingine kikubwa zaidi au kutanuka zaidi
assuming that all other costs remain constant (nadhani huyu mtu mwenye mtaji wa 5000 ni aidha mama wa nyumbani au mtu anakaa kwa ndugu au mfanyakazi ambaye kipato chake hakitoshi kuweza kubaki na mtaji mkubwa zaidi ya huu)
Naona wengi hawaamini lakini ujasiriamali ni kubuni biashara kulingana na malighafi ulizonazo au unazoweza kutumia bila gharama yeyote au kwa gharama ndogo sana. Mtu wa nyumbani au mama anaangalia jiko, vyombo nk wanavyotumia hapo kama malighafi hivyo anahitaji unga, mafuta nk ili aanze biashara. Ndiyo mfano wa ndg Mengi aliiangalia uwani kwake akaona anaweza kuanzia kiwanda, wakati kwa alipyepanga ingebidi akodi yard ili aweke hicho kiwanda.
Mtaji kwa uelewa wangu ni hela nje ya matumizi yako ya kila siku, hivyo akisema 5000 hamaanishi chakula, mavazi na malazi itoke hapo kabla sijazalisha na kuwa stable walau kwa mwezi 1 au 3.


 

Umeandika as if una uhakika wa kuuza kila siku?!
 
Mazingira ya kutengeneza na kuuza hiyo juice nayo inanipa tabu!
 
Nadhani anaanza kwa kusindika kwa mkono ubaridi anadandia kwa wazoefu , kuhemsha anadandia jiko la mama ntilie alitye karibu n.k. otherwise haitoshi 5000 kuanza nayo
 
Je kwa asiyekua KKB(Kulakulala Kwa Baba)?

Kaka badlisha avatar; maana naona sku hizi umeanza kufanana nayo..hahahaa!
Nadhani ni vizuri ukarudia kusoma heading ya Ndyoko; amesema hiyo elf5 inaweza kumtoa yeye ambaye ni kula kulala katika mazingira yake kivyake, kama wewe siyo kula kulala unatakiwa ujiongeze kivyako ili hyo elf5 ikutoe, ukipenda unaweza kwenda kuirambia ugimbi ili upunguze mawazo!:yawn:!
 

Ungekuja na wazo panufu mkuu ungekuwa umesaidia wengi kuliko kuponda tu bila kutoa ushauri ulio wazi na mpana. Tunajaribu kumsaidi ndugu yetu Ndyoko hapa yeye anadai ana mtaji wa buk5 tu na anataka imtoe na aendelee kubaki mjini na hatimae kutoka, sasa wewe kama unamshauri arudi shamba kulima itakuwa vizuri kumwekea mchanganuo wa kilimo kwa hiyo buku5, kumbuka kuwa hana ardhi wala jembe!!! Karibu.
 

AMOEBA umerudi,nashukuru sana AMOEBA umeanza kupata mwanga kua elfu tano haiwezi kununua hata jembe kwa kweli mie hua nashukuru sana napomwelimisha mtu halafu akaanza kunielewa,ndio maana AMOEBA nikakuambia labda elfu tano ya kimarekani ili aweze kununua angalao kajishamba na jembe na kabalance kabaki ka emegency lakini mwanzoni ulipinga sana lakini naona kadri tunavyozidi kukuelimisha unaanza kutuelewa.
 

Ha ha haa haaaaa AMOEBA unavituko kweli.
 

Kaka haujajbu hoja!! Mdau ametoa mchanganuo wake vizuri kabisa, na mifano HALISI tumekuwekea hapa, bado unabisha tu!....nimeanza kupata mashaka na wewe!:A S embarassed:
 


Katika Dunia ya wajasirimali michango kama hii haitakiwi kabisa,

Mkuu mjasiriamli huwa ana strategies nyingi sana za biashara na moja ya strategies ni kuona aanzishe vipi business kwa mtaji mdogo?

Hapa mjasirimali inabidi akae chini na aumize kichwa atafanyeje.

MKUU NDO MAANA KATIKA STRATEGIES ZA KIJASIRIAMLI KUNA HAYA,

1. Kuanzisha biashara ukiwa nyumbani/ offisi inakuwa ni chumba unacho ishi wewe,- hii ni mbinu ya kupunguza ghalama na usiniulize hicho chumba kitakuwa hakilipiwi, hapa ni kwamba kabla ya kuingia kwenye ujasiriamli hicho chumba ulikuwa unakilipia vip?

2. Kutumia vifaa vyako ulivyo nunua kwa kazi tofauti. mkuu wewe unaweza ukawa unagheto lako na unataka kuligeuza gheto lako la chumba kimoja kuwa gest na na tiyali ulikuwa na kitanda ulicho kuwa unalalia so hapa tiyali unakuwa umetumia strategies nzuri sana,

3. Kuwa kila kitu- wewe ndo meneja, mhasibu, mkurugenzi, msambazaji, afisa ugavi, afisa masoko, na kazalika so hapa ili kuipeka ghalama wewe una kuwa kila kitu mpaka hapo utakapo simama vizuri ndo uweze kuajiri wafanyakazi,

4. Kuangalia wapi uatapata vifaa vya bure vya kufanyia kazi, hapa mkuu mtoa maada anaweza kuwa atatumia vifaa vya rafiki yake, ndugu au jirani yake kwa kuanzia, so hii mkuu ni mbinu ya kijasiriamali.

SO WA KUU MSISEME HAIWEZEKANI NA KAMA WEWE NI MWAJIRIWA UNASUBILIA MWISHO WA MWEZI HAITAKAA 5000 IFANYE BIASHARA DAIMA, NA KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA HAITAWEZEKANA, ILA KAMA WEWE NI MJASIRIMALI INAWEZEKANA SANA
 
Nadhani anaanza kwa kusindika kwa mkono ubaridi anadandia kwa wazoefu , kuhemsha anadandia jiko la mama ntilie alitye karibu n.k. otherwise haitoshi 5000 kuanza nayo

Mkuu hizo zote ni moja ya mbunu za kijasiriamli, huwezi anzisha biashara bila kuwa na mbinu mbalimbali, la sivyo makampuni makubwa ya dunia kwa sasa yasingekuwepo kabisa
 


Hii nilikuwa sijaisoma, UNA MAWAZO POTOFU! Mifano niliyokupa mimi si ya kusadikika, ni real life scenario kaka, ELEWA! Sifahamu Mengi alikotoka, lakn suala la kusema alipiga NBC linaonesha kuwa uko low sana kaka. Hata hzo deals huwezi kupata kizembezembe tu, lazima wadau wakuone we mchakarikaji!
AMKA!
 

Mkuu Sijakupata kabisa, kila biashara inawezekana kukua na ikawa kubwa sana.

1. Mama lishe anaweza kupanua biashara yake na akamiliki migahawa mikubwa ya chakula east and central Africa, tatizo wanakosa mbinu za kijasirimali wanakosa Vision na ndo maana biashara zao zinashindwa ku graduate kutoka small to medium na kutoka medium to big one.

2. Machinga mutembeza viatu anaweza kugraduate na kuwa na maduka makubwa sana ya kuuza viatu, anakosa mbinu za kijasiriamali ndo maana anashindwa ku grdaute kutoka hapo alipo kwenda hatua nyingine.

3. Jamaa muuza juice anaweza kugradute na akamiliki kiwanda cha kusindika juice na akawa anauza hadi ulaya, mkuu huyu mtyu anakosa mbinu za biashara za kumwezesha ku sogea kutoka step moja kwenda nyingine,

4. Mkulima, anatakiwa amove kutoka hapo alipo, amiliki shamba kubwa na vitendea kazi vyote hii ni pamoja na kuwa na kiwanda chake mwenyewe cha ku process na kupak,

MKUU WAKULIMA UNAO SEMA MBONA WENGI WAO WAKO HAPO WALIPO MIAKA NENDA RUDU? JE WANATOFAUTI GANI NA WAMACHINGA?

WOTE WANAKOSA MBINU ZA KUWEZESHA BIASHARA ZAO KU GRADUATE KUTOKA BIASHARA NDOGO KWENDA YA KATI NA HATIMAYE KUBWA

So mkuu biashara ya aina yoyote inaweza kumfanya mtu akawa bilionea mkubwa sana tatizo watu wetu wana laki mbinu za kuwa fanya kusogea ndo maana miaka nenda rudi utakuta ni umachinga tu au ni mama lishe miaka nenda rudu,
 


Mkuu nimeipenda sana hii, na niseme ndo moja ya character za Entrepreners wote, huyo Dada hakuwa na hata sh 100 ila nyumbani kulikuwa na vitendea kazi akaamua kutumia hivyo vya nyumbani kuanzisha car wash,
Hiyo ni mbinu ya kijasiriamli kabisa na wajasiriamli wakubwa wa dunia wlitumia mbinu hii kutoka.

Kuhusu point yangu ya kwanza, ni kweli ila ni mejarubu tu kuonyesha ni jinsi gani inawezekana ila kama yeye ni profit oriented hiyo ni up to him
 

Nimeona nimeipenda nilijaribu na nikaweza
 
Hii kitu inawezekana kabisa siyo lazima uanze na mtaji mkubwa. mimi mwenyewe nilianzisha biashara nikiwa na mtaji wa 18,000,000/= baada ya mwaka mmoja na nusu nikapata hasara ya 4,000,000/= nikabakiwa na 14,000,000/= hii ilinipa changamoto sana nikaamua kuchukua 13,000,000/ nikanunua kiwanja na kujenga kibanda cha vyumba viwili na kuanzisha biashara kwa mtaji wa shilingi 500,000/ tu na kwa sasa naingiza 700,000/= kila mwezi kwa mtaji wa 500,000/= nilioanza nao.Mimi naamini kabisa hata hiyo 5000/= inaweza kukutoa kama uko committed kwa mfano wauza mchicha wananunua kwa shilingi 50/= kila fungu na kuja kutuuzia kwa shilingi 100/= anapata faida ya 100%.
 
Kuna watu hawaamini ktk hili,lakini kuna watu wameanza biashara wakiwa mikono mitupu kabisa na leo wana mitaji mizuri.Wakati mwingine nguvu/afya/kujua ni mtaji tosha kama uko ktk mazingira ya kula kulala.

Wakati nasubiri matokeo ilibidi niombe viazi home kama debe moja kisha nibebe kwa kichwa km 35 ili nikauze,debe hilo likiuzwa sh 150/. Mtindo uliokuwa ukitumika enzi hizo ni kwamba unalipwa nusu kisha nusu unaifuata siku nyingine. Kwa hiyo nilipiga safari kama kumi hivi na nikajipatia 1,500/. Enzi hizo 1500 ilikuwa ni ada ya secondary ktk shule binafsi.

Baada ya kupata hiyo hela,ilibidi home wasijue,nikabadili biashara, nikawa nakusanya mayai kijijini na kupeleka kimji cha jirani. Mjasiriamali lazima uwe mbunifu sana kwa kuangalia mazingira uliyo nayo.
 
Hili nalo neno
 
Kama biashara zingekuwa rahisi kwa mtindo huo sidhani kama kungekuwa na "MASIKINI"

ni maskin kwa sababu hata mind zetu ni maskin kwa kufikiri, acheni kukatisha wenzenu tamaa kuna watu wanakaa home wana kila kitu kama hizo vitendea kazi lakini anambwela tu kutwa kubadilisha movies na series, kula kulala bure angemwambia dingi me naanzisha kuuza juis nadhani pia angesapotiwa home

biashara ni nia na commitment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…