Unachokiongea KOMMANDO kina ukweli ndio maana nimekugingea like (BUT hapo kwenye RED unapingana na title, kwani jamaa anataka kutoka), lakini umebase kwenye lecture zaidi ya hali halisi inayotokea site (soma saiti). Wakati nafanya mafunzo ya ujasiriamali hayo maneno niliyasikia sana, but ukimtizama mkufunzi anayekufundisha utagundua haamini anachokisema au hajui hali halisi ya site.
Sasa kwa kuwa wengine tulikuwa ni watu wa Site kwa muda mrefu tulikuwa na advantage kidogo ya kuwasumbua walimu wetu, ingawa nilijifunza mengi lakin vitu vingi nilivyotegemea kuvipata sikuvipata. Ni suala hili ndilo lililonifanya nitafute Mentor, ambaye yupo juu zaidi yangu ili nijifunze mambo halisi ya Site through what they call Tacit knowledge. Elimu hii haina cheti, lakin mchango wake kwa mtu yeyote ni mkubwa sana, nadhani ndio maaa watanzania wenye Asili ya Asia wanafanikiwa sana.
Mambo mengi ambayo sikuyapata darasani, niliyapata Site kwa Mentor wangu na baada yakuona nimekubuhu aliniacha niendelee na biashara zangu. Mambo niliyojifunza huko site ni tofauti sana na ya darasani, na ndio ninayokutana kila siku kwenye ujasiriamali wangu, hivyo naweza kukabiliana nayo. (Mpaka nilipata wazo la kuanzisha darasa litakalokuwa facilitated na real entrepreneurs, na litakuwa promoted na hii slogan WHAT IS NOT TAUGHT IN BUSINESS SCHOOL).
Nakumbuka wakati huo ninasomea ujasiriamali, tulikuwa tunafundishwa kwamba, fedha si chochote kwa mjasiriamali halisi, kama ulivyosema wewe na kweli nakubaliana na hilo kwa kiasi fulani, na hapa nitoe mfano labda utawa motivate watu fulani,
"Kuna binti aliamua kuingia kwenye car washing business, kwa kuanza na kuosha gari la baba na mama yake baada ya kuwashawishi wasiende tena car wash za nje. Resources zote zilipatikana nyumbani tena bure, hivyo akawa anatengeneza 8000 per day, baada ya mwezi mmoja akaamua kuwazungukia majirani zao wenye magari, akapata hapo wateja wengine wawili... biashara iliendelea kuingiza mapato na wateja wapya ikabidi binti aajiri watu wengine, na baada ya muda akanzisha CAR WASH kwani alishakuwa na fedha za kutosha, knowhow na soko"
Lakin mimi nasema hiyo ni kwa mazingira fulani tu, huku site mimi nilifundishwa mambo manne in getting more work done nayo ni motivation, know-how, capital and outlet. Na hapa query inayojitokeza ni kwenye hiyo capital (Tsh. 5000). Issue kwamba itatosha au haitoshi na mtu atatoka kwa muda gani, nadhani tuyaachie mazingira kwani yanatofautiana.
Ila kwangu mimi nasema mazingira hayo yataathirika sana na UMRI wa muhusika, majukumu yake, matumizi yake, soko lake na sehemu alipo. Until then ndio utaweza kutoa conclusion kuhusu huo mtaji.