Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!

mkuu nakubaliana NA mtoa mada elfu 5000,ni kubwa sana, MM japo sikua serious nilinunua kifaranga cha mtetea ambacho hakijaanza kutaga(huwa napendaga sana kuku) nikawa nakifuga home chakuka kilikua mabaki ya msosi home ambayo yalikua yanatosha kikuku kimoja kilivyo zoea nikawanakiachia nje mtaani jioni kinarudi,miezi ikapita kikawa kinataga jogoo alipata huko huko mtaani, nikajastuka simuoni kumtafuta nikakuta kamejificha kanatamia, nikawa sina uhakika wa mayai coz jogoo sikuwa nalo,baada ya mda kaja na vifaranga nane nikashangaa na kufurahi pia, hapo nikaenda tandale pumba ndoo 1 sh 2000 nikavitunza saiv wapo wengi sana home. Nauza mayai tuu nayawekaga dukani kwa bi mkubwa, trey 15000 ni reja reja. Saivi. nipo mbali nipo chuo Ila naambiwa wapo vizuri coz nilishawajengea kibanda.
 
ndyoko huo ni uwongo
sukari robo kwa lita 5???hata ukitumia kk(kimoja kimoja)haikolei
unaijua KK au unakurupuka amu au ndo unachangia.KK ni kiboko maana vijiko 5 vya ubwabwa vinakoleza maji lita30 ni kiboko ya chumvi..
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli kabisa inatosha!! Mimi ni mwanafunzi wa chuo flan hapa dsm!! Me nilianza na mtaji wa 14000/= hivi sasa nalaza kwa cku faida kama 10000/= hapo nimeshatoa gharama za msosi kila kitu!!

UKIJITUMA INAWEZEKANA!!!
 

Hapo kwenye nyumba ndo utakapofilisikia. Kuza mtaji nyumba yako ya kuishi itokane na faida ya biashara.
 

Mi nakubaliana kabisa na ww, achen kukatishana tamaa jaman cha msingi nikutoa option ya kufanya kitu kingne ambacho kina uhitaj mdogo wa vitendea kazi out from hyo yenye gharama kubwa from ze same amount of money
 
... Tuache visingizio jamani. We uko radhi utumie laki moja kula nyama choma na bia badala ya kuanzisha kibanda kidogo cha juisi. Kama unaogopa kuuza wewe mwenyewe, weka kijana akuuzie hizo juisi basi.

"Jana nimetumia zaidi ya laki unusu. Leo hadi sasa saa10 na dk 10 nishatumia laki na elfu themanini. Usiulize mapato yangu maana haviendani. Nakula akiba!"

Mkuu, hapo nawakilisha jamii pana ya 'wasomi' wenye ajira zao za kudumu. Hivi angeamua kuajiri hata nduguye asiye na kazi kwa mtaji huo wa laki 3, miaka 10 ijayo angekua wapi? WaTz wanahitaji upako wa kijasiriamali. Wengi wataendelea kuhadithia tu utajiri 'wetu' ilhali hata wao wangeweza kuwa upande huu.

Kuna chalii mmoja alikua anauza bidhaa za umeme kimachinga. Kakua hadi kuwa na kiduka uchwara. Kakua hadi anasafiri kwenda China. Kiduka kimekua japo muuzaji ye mwenyewe akisafiri anafunga.

Majuzi ananiomba ushauri eti anataka kununua Verossa. Nimemwambia aache huo ujinga. Gari litamgharimu sana. Hakuniskia. Kajitutumua kanunua subaru Forrester. Si unajua watoto wa Arusha wanavozipenda!

Hapa namuhesabia kufilisika kwake. Na nitainunua hiyo gari kwa chee maana anavyoitunza! Halafu nitaiuza cha juu kumuumiza roho ajifunze vipaumbele. Navyoandika, naye keshajiunga na kundi linaloilalamikia Januari utadhani hakujua inakuja!!

Bottom line. 5000 inatosha kwa mwenye ujasiri wa amali. Mitaji mingine ni kama ujuzi, mtandao wa wateja/watu, uaminifu, kauli tamu, n.k.
 
Naona Vipofu Mnaongozana kuvuka Barabara!
Hapo Bado Hujasolv Tatizo La Barafu,
Vitendea Kazi
Mgambo
n.k
Sio Rahis Kama Mnavyozani

Jigo, vitu vingine mali kauli. Mtaji huo wa 5000 ni wa hela. Upungufu mwingine tumia mbinu za kuzaliwa kuvipata au azima. Barafu tafuta jirani mwenye friza, ugandishe kwa ahadi ya kumlipa kitu kidogo biashara ikianza. Na hivi luku ghali, wengi hawakatai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…