bepari la kichaga
JF-Expert Member
- Dec 21, 2014
- 528
- 516
mkuu nakubaliana NA mtoa mada elfu 5000,ni kubwa sana, MM japo sikua serious nilinunua kifaranga cha mtetea ambacho hakijaanza kutaga(huwa napendaga sana kuku) nikawa nakifuga home chakuka kilikua mabaki ya msosi home ambayo yalikua yanatosha kikuku kimoja kilivyo zoea nikawanakiachia nje mtaani jioni kinarudi,miezi ikapita kikawa kinataga jogoo alipata huko huko mtaani, nikajastuka simuoni kumtafuta nikakuta kamejificha kanatamia, nikawa sina uhakika wa mayai coz jogoo sikuwa nalo,baada ya mda kaja na vifaranga nane nikashangaa na kufurahi pia, hapo nikaenda tandale pumba ndoo 1 sh 2000 nikavitunza saiv wapo wengi sana home. Nauza mayai tuu nayawekaga dukani kwa bi mkubwa, trey 15000 ni reja reja. Saivi. nipo mbali nipo chuo Ila naambiwa wapo vizuri coz nilishawajengea kibanda.