Unahitaji elimu ya uchumi aisee. Thamani ya pesa haihusiani na ukubwa/udogo wa uchumi wa nchi, tafuta maarifa kabla ya kucomment.
Fedha ya Kuwait ina thamani ×3 ya fedha ya Marekani USD kwahiyo hapo utaniambia uchumi wa Kuwait ni mkubwa kuliko USA!?
Tukubaliane kitu kimoja kuwa na pesa ina nguvu haina maana uchumi wako ni bora kuliko aliyechini. Nguvu ya pesa sio kigezo. Maana kama ingekuwa ni hivyo basi leo hii Oman, Kuwait na Bahrain tungeseme uchumi wao mkubwa kuliko Saudia, UAE na Qatar. Leo hii tungesema Oman uchumi wao mkubwa kuliko USA au China. Sababu dola 100$ ukichange Oman unapata Riyal 36 hivi.
Djibout hapo pesa yao ina nguvu kuliko yetu kwa hiyo uchumi wao ni bora? kwanza pesa yako ikiwa chini na unazalisha sana una take advantage ya mwenye pesa yenye nguvu sababu itakuwa bei rahisi kwenye soko shida ni kama unanunua kila kitu. China mpaka leo ugomvi wake na USA ni kuwa US anadhani China makusudi tu wanaishusha pesa yao dhidi ya US ili biadhaa zao zionekane cheap. Uchumi una mambo mengi ya kupima lakini ni kweli Kenya bado wametupita kwenye uchumi lakini tusipime kwa Shilling.