Sh178M kwa Polisi Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano: Serikali Yaanza Kulipa Officers Walioathirika

Sh178M kwa Polisi Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano: Serikali Yaanza Kulipa Officers Walioathirika

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Zaidi ya Sh178 milioni zimelipwa kama fidia kwa maafisa wa polisi waliofariki au kujeruhiwa wakiwa kazini wakati wa maandamano na protests nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Panel of Experts on Compensation of Victims of Human Rights Violations, angalau maafisa 178 wamepokea malipo katika phases III, IV na V za compensation programme.

Maafisa wawili waliofariki walipewa Sh3 milioni kila mmoja. Afisa mmoja aliyepata aggravated injuries alipewa Sh2.5 milioni, huku wengine 11 wenye majeraha makubwa wakipokea Sh1 milioni kila mmoja.

Maafisa wengine 60 wenye majeraha ya wastani walipewa Sh500,000 kila mmoja, huku 104 waliopata majeraha madogo wakilipwa Sh50,000 kila mmoja.

Lakini polisi si kundi pekee linalolipwa.

Panel inayoongozwa na Prof Makau Mutua inasema hadi sasa imeprocess claims 1,083, zinazohusisha vifo, majeraha, sexual violence, economic losses na madhara mengine yanayohusishwa na maandamano. Claims nyingine 139 za wafanyabiashara wadogo na informal businesses pia zimelipwa.

Kwa ujumla, zaidi ya Sh1.014 bilioni tayari zimelipwa kupitia programme hiyo. Panel inasema kila claim inafanyiwa verification na categorisation kabla ya malipo kuidhinishwa.

High Court iliagiza Sh105 milioni itengwe na isitumike wakati kesi inayohusu victims wa torture, abductions na enforced disappearances ikiendelea. Panel imethibitisha kuwa fedha hizo zimewekwa kando kusubiri uamuzi wa kesi.

Court records zinaonyesha petitioners walikuwa na wasiwasi kwamba compensation process ingeweza kukamilika huku victims wa enforced disappearances wakiachwa nje.
 

Attachments

  • eastleighvoice-co-ke-2026-september-15-183702.webp
    eastleighvoice-co-ke-2026-september-15-183702.webp
    197 KB · Views: 23
Back
Top Bottom