Shaaban Robert Angesemaje Kuhusu Mjadala Wa Katiba...?

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,246
Ndugu zangu,

Kama Mwanafasihi na mshahiri mahiri Shaaban Robert angelikuwa hai ,basi, kwenye hili la mjadala wa Katiba yumkini angetamka;
" Turufu huenda kwa mchezaji...!"

Maana, tunaukumbuka mjadala ule kwenye simulizi ya Mfalme Rai. Ni juu ya mjinga na mwerevu. Naam, mkulima ni mjinga na mwenye duka ni mwerevu. Kwa nini kuna wenye kuamini hivyo?

Ndio, wenye kuamini hivyo wanadhani, kuwa kwa vile mkulima anashika jembe tu, basi, hana halijualo.

Na kwa vile mwenye duka anafanya kazi ya kuhesabu pesa, basi ni mwerevu.

Lakini, kama mwenye duka naye hupata hasara, ina maana nae ni mjinga?

Na ni mkulima anayesemwa kuwa ni mjinga ndiye mwenye kuwalisha wengine, wakiwamo wafanyabiashara.

Na kwa vile wakulima wenye kusemwa kuwa ni wajinga ndio walo wengi, basi, hekima na busara ni kwa Mfalme kuhakikisha kuwa hao ndio walio nyuma yake.

Lililo jema ni kuwasikiliza. Maana, turufu siku zote huenda kwa mchezaji.

Maggid.
Iringa.
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
shaban robert anaingiaje kwenye mjadala huu wa CCM kupora mchakato wa katiba??
 
Unafikiria habari za wafu utafikiri unatoka kuzimu! Sema wewe unasemaje juu ya mjadala wa katiba ili tuchangie!
 
Kwani shabaan robaer alikuwa nani zaidi ya maishiri..sidhani km ni thinker kihivyo...
 
Well said Mjengwa,
Nadhani leo umenena.

Back
Top Bottom