PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mgombea Udiwani wa Kata ya Mwendakulima, iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaban Mikongoti, amewaahidi vijana wa kata hiyo kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Akizungumza leo Septemba 21, 2025, wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika katika Mtaa wa Mwime ya Makungu, Mikongoti amesema Kahama ni kitovu cha uchumi wa mkoa wa Shinyanga hivyo kupitia mikopo hiyo, vijana wana nafasi kubwa ya kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayowainua kimaisha.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini kwa tiketi ya CCM, Benjamin Ngayiwa, amewahakikishia wananchi kuwa iwapo wataichagua CCM katika uchaguzi ujao, changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hiyo zitatatuliwa, ikiwemo tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya na ubovu miundombinu barabara.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, aliwataka wananchi waendelee kuiamini CCM kwa kuwa ni chama chenye dira na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama na Tanzania kwa ujumla.
Uzinduzi huo wa kampeni umehudhuriwa na mamia ya wakazi wa Kata ya Mwendakulima na mashabiki wa CCM, ambapo pamoja na hotuba, kulikuwa na burudani mbalimbali za ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya.