Shaban Nonda alitufanya uchochoro, Sasa tumekuwa barabara

Shaban Nonda alitufanya uchochoro, Sasa tumekuwa barabara

Mavotah

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2013
Posts
280
Reaction score
119
Ni miaka 21 imepita tangu Shabani Nonda kuelekea South Africa na baadae kufanikiwa kuvuma sana Ulaya na Dunia nzima. Baada ya Nonda kufahamika tulitetegemea milango itafunguka kwa soka letu na wachezaji wetu kujielewa na kupambana ili kupata mafanikio kama ya Nonda lakini imekuwa ni shida. Mwezi uliopita mganda Emmanuel Okwi amepata nafasi ya kwenda kuanza maisha mapya Denmark hii ikiwa ni nafasi ya pili baada ya Eteol Du Sahel kuisha kwa mizwengwe, Sasa tujiulize Okwi anondoka mara ya pili wazawa kuna hata mmoja anaeonyesha nia?. Labda tuseme ya Okwi makubwa vipi ya Kpha Sherman kacheza mechi 27 na kufunga magoli 6mengi yakiw sio ya ligi Jana kakamilisha mkataba wake na Mpulanga black Acers timu ya ligi kuu PSL bila ya kufanya majaribio, amepimwa afya tu kasaini mkataba. Sasa tujiulize mfungaji bora wa Tanzania msimu uliopita Simoni Msuva alishindwaje majaribio wakati Sherman amepita? na pia vipi kuhusu mchezaji anaeaminika ni kiungo bora Sasa nchini Jonas Mkude nae siku mbili tu karudi tatizo liko wap? Au shida ni mawakala maana naambiwa wakala ndo anamtangaza mchezaji kama bidhaa sokoni na pia kumhudumia tusije tukawa tunawalaumu bure kumbe wanapelekwa sokoni na wahuni tu kama yale ya Kapombe kwenda kushindia maji Ufaransa alafu akakabane na wakina Cisse. Tujiulize jamani tutatue tatizo tusiwe njia tu.
 
Hivi kweli ukimtazama Mkude unaridhika kabisa kuwa ni mchezaji bora wa kucheza nje ya Tanzania? jamani tuwe wakweli, magazeti yetu yanawapaq sifa ziszo na maana.
 
Mbona uncle haujamtaja???Au naye hajafanikiwa huko south tena YATUPASA KUSHANGAA SN KWANI NGASA YULE KTK UBORA WAKE ALIZUNGUKA HAPA HAPA Young,simba,azam na young!West ham siku moja tu akarudi.!!
MAISHA NI BAHATI.YOUNG WALIMUACHA KIIZA HILI SHERMAN APATE NAFAS LEO HUYOOO SOUTH.
Bora yanga inafanywa BARABARA KULIKO KULE MTAA WA PILI AMBAPO NI airport.
 
KUZUNGUMZIA PROFESIONAL PLAYERS TANZANIA NI NGUMU KUMEZA KWA WADAU WA SOKA NCHINI.
Wachezaji wengi hudanganywa sana na magazeti ya bongo...hasa wakifanikiwa kuchezea Simba na Yanga....wakienda mashindano ya kimataifa wapi low class kweli
 
wachezaji wa tanzania sio wapambanaji na simba, yanga na azam zinawadanganya sana. samata, ulimwengu, luizio ni mfano wa wachezaji wapambanaji. kuna mtu kasema eti kapombe alikuwa anashindia maji hivi anajua wachezaji wa afrika magharibi kwanza wanafikajefikaje ulaya na pili wanapambanaje ili kupata nafasi ya kucheza mpira ulaya. jaribu tu kufuatilia historia ya jay jay okocha kufika ulaya na kuanza kucheza mpira. wachezaji wetu wana bahati sana ya kupata nafasi kwenda kufanya majaribio lakini wanashindwa kutokana na kukosa roho ya kiupambanaji. jiulize leo jerry tegete anajuta kiasi gani kwa kitendo chake cha kurudi kuwahi mechi ya simba na yanga na kuacha kumalizia majaribio au ngasa angekomaa baada ya kutemwa west ham leo angekuwa hata lique 1 ufaransa.
 
Wachezaji wa Tanzania sio wahangaikaji wa kutafuta mafanikio, wakichezea Simba na Yanga wametimiza ndoto zao. Miaka ya tisini wachezaji wa kutoka Afrika ya magharibi walikuwa wanaruka maboda kwenda kutafuta timu S.A. Ulaya kuna wachezaji wa kutoka huko wanasota na hali ngumu kutafuta mikataba. Samuel E'too mwenyewe mafanikio hayakuja tu hivi hivi, first day anaingia Ulaya hakukuwa na mtu wa kumpokea airport, hakujua lugha za watu na mfukoni alikuwa hana kitu.

Tuache kulialia hatuna bahati, tujifunze kuwa na mazoea ya kujituma ili tukipewa nafasi tuonyeshe uwezo. Talent tu haitoshi bila kujifua. Mchezaji anayetaka mafanikio hawezi kusubiri saa 10 jioni akapige stori na kocha. Be inspired jamani, si mnasikia stori za kina Ronaldo, Mayweather na wengineo, kujifua ndio siri ya mafanikio, waganga wa kienyeji wasanii tu.
 
tatizo kubwa ni waganga wa kienyeji, mchezaji kila siku anapigwa chale, anaogeeshwa njia pandda unategemea nini
 
wachezaji wa tanzania sio wapambanaji na simba, yanga na azam zinawadanganya sana. samata, ulimwengu, luizio ni mfano wa wachezaji wapambanaji. kuna mtu kasema eti kapombe alikuwa anashindia maji hivi anajua wachezaji wa afrika magharibi kwanza wanafikajefikaje ulaya na pili wanapambanaje ili kupata nafasi ya kucheza mpira ulaya. jaribu tu kufuatilia historia ya jay jay okocha kufika ulaya na kuanza kucheza mpira. wachezaji wetu wana bahati sana ya kupata nafasi kwenda kufanya majaribio lakini wanashindwa kutokana na kukosa roho ya kiupambanaji. jiulize leo jerry tegete anajuta kiasi gani kwa kitendo chake cha kurudi kuwahi mechi ya simba na yanga na kuacha kumalizia majaribio au ngasa angekomaa baada ya kutemwa west ham leo angekuwa hata lique 1 ufaransa.
Kupambana kupo lakini inategemea umetokea katika mazingira gani, wakala anamchukua mchezaji Simba au Yanga mshahara wa chini laki sita bado kuna posho ndogo ndogo anampeleka Ufaransa akacheze timu ya akiba bila malipo yoyote na Bongo kaacha familia na bado club za bongo zinamfuata kwa day zuri, kiukweli hata ni mimi narudi. Tatizo hatuna mawakala waliotayari kumgharamia mchezaji, kwa upande mwngne tusilaumu tu wachezaji
 
watu wengi hawajui kuwa yale maboti yaliyotengenezwa kienyeji yanayovuka mediterenean na wahamiaji haramu ndani yake pale kuna watu baada ya miaka 3 au 4 tutawasikia wapo epl, bundesliga n.k. sembuse hawa wa kwetu wanaondoka airport paspoti ina viza kila kitu kiko safi. wachezaji wetu akili zao zimeishia simba, yanga na azam basi na waandishi wa habari wakisha wapamba kwenye kurasa za mbele za magazeti basi. nafikiri umefika wakati sasa kwa wachezaji kubadilika waanze kupamabana kutafuta nafasi za kucheza nje na waanzie afrika kusini au nchi za scandnavia taratibu watajikuta wameshafika ulaya. na wasisubiri mpaka umri uended sana.
 
Back
Top Bottom