Shabani Kaoneka alalamika Mandonga kupambwa zaidi yake aliyeshinda pambano

Shabani Kaoneka alalamika Mandonga kupambwa zaidi yake aliyeshinda pambano

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mabondia Karim Mandonga na Shaban Kaoneka wamerudi tena kwenye headlines kufuatia kauli ya Shaban Kaoneka aliyoitoa jana akizungumza na Wasafi.

"Mandonga amepata bahati kuliko mimi, waandishi wa habari wakati mwingine mnakuwa wanafiki, mimi niliyeshinda nakuwa masikini aliyepigwa anakuwa tajiri,"

Kauli hiyo imemuibua Mandonga Mtu Kazi ambaye hivi karibuni amelamba madili mbalimbali!

"Dah Shabani ndugu yangu me naamini kabisa ridhiki inatoka kwa mafungu na kwa muda maalumu alieupanga Mungu suala la nani afanikiwe nani aishie njiani ni majukumu ya Allah mimi na wewe hatupaswi kumlaumu mtu yoyote yule.

"Katika tasnia hi ya mchezo wa ngumi na watu wa media kiujumla hata mimi sijawahi kuwaza kwamba ipo siku nitasimama kama SUPERSTAR MKUBWA but all in all tujfunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo. KAMA IPO IPO TU"
 
Mandonga anajitambua pia ana meneja mahiri anayejiongeza.

Amebadilisha scenario ya boxing kwa namna alivyojiongeza kabla na baada ya pambano lao. Fuatilia trends za Mandonga kabla ya pambano na soon baada ya kuchezea kichapo utagundua kwamba alionesha kutojali matokeo kama mkwamo bali aligeuza fursa na akaonekana kwenye mizania ya matangazo akaanza kutumika.

Kaoneka alipaswa kuwa na meneja mahiri lakini kwa sasa anahitaji daktari wa saiklojia asije akaua mtu
 
Watu wanawekeza kwenye pesa. Sasa kama Mandonga anarudisha pesa kwanini wasiende? Hata hivyo bila Mandonga huo mchezo wao ungekuwa na umaarufu?

Kama ni mjanja atumie jina la Mandonga kujipa umaarufu. Hapo akisema mimi Mandonga naweza mchapa hata mbele ya mkewe kama huamini aombe rematch halafu aje na mkewe halafu Mandonga aombe rematch atazidi kujipa umaarufu na pambano litafatiliwa maana watu wanapenda siasa za aina hiyo na mke wa Mandonga naye atakuwa famous.
 
Hii inanikumbusha kipindi kile fid q alipompa stive nyerere usemaji wa chama cha wanamuziki,baadhi yao wakapinga na toka pale na chama chenyewe sijui kama bado kipo
 
Na yeye aache wivu. Kwanza anatakiwa kumshukuru hiyo Mandonga kwa kumrejesha kwenye mchezo wa masumbwi! Maana alishastaafu hapo kabla.
 
Mandonga mtu wa kazi Kaoneka atulie tu kila mtu na bahati yake.
 
Nimeona video ya kaoneka akilalamika mandonga kupata pesa licha ya kuwa alimtwanga. Haya ni malalamiko ya kitoto sana kwa Bondia aliyeshinda pambano muhimu kama ile.

Wanamichezo na wasanii wa bongo wamezembea sana kwenye swala la branding wanatumia majina makubwa kunywa bia na kuopoa mademu badala ya biashara.

Kwanini hamjimfunzi kwa the powerful brand DIAMOND platnumz jamaa sio mwanamuziki mzuri lakini powerful and rich sababu ya brand

Amkeni
 
Nimeona video ya kaoneka akilalamika mandonga kupata pesa licha ya kuwa alimtwanga. Haya ni malalamiko ya kitoto sana kwa Bondia aliyeshinda pambano muhimu kama ile...
Some time Maisha Ni ufara Sana .......jamaa kapigwa lkn anapata headlines kubwa kuliko hata aliyempiga[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Some time Maisha Ni ufara Sana .......jamaa kapigwa lkn anapata headlines kubwa kuliko hata aliyempiga[emoji23][emoji23][emoji23]
Kitu ambacho Hana Mandonga Ni Mkanda tu😂, story ya Mandonga na Kaoneka Ni Kama mimi katika real life,Nina degree lakini wanangu walioishia form four wameoa, Wana gari, wanakazi nzuri za kuajiriwa au kujiajiri ,wengine wapo Dubai, India, Mimi nipo tu hapa Sina kitu
 
Back
Top Bottom