Shabani Kaoneka alalamika Mandonga kupambwa zaidi yake aliyeshinda pambano

Shabani Kaoneka alalamika Mandonga kupambwa zaidi yake aliyeshinda pambano

Ndio ujue kama Bongo wengi sifuri. Mtu anaongea kitu kwa sababu hana fikra, anazungumza kitu hakina mantiki.

Mandonga kilichomuweka pale ni mdomo wake na kipigo alichopewa. 😂, mamdonga kawa maarufu toka pambano lake lile akula mkono mmoja tu chalii😂
 
Mandonga kama Mandonga

Kila mtu ana namna ya kutoka wakati ukifika..........
 
Mandonga anajitambua pia ana meneja mahiri anayejiongeza.

Amebadilisha scenario ya boxing kwa namna alivyojiongeza kabla na baada ya pambano lao. Fuatilia trends za Mandonga kabla ya pambano na soon baada ya kuchezea kichapo utagundua kwamba alionesha kutojali matokeo kama mkwamo bali aligeuza fursa na akaonekana kwenye mizania ya matangazo akaanza kutumika.

Kaoneka alipaswa kuwa na meneja mahiri lakini kwa sasa anahitaji daktari wa saiklojia asije akaua mtu
Kwanza hata pambano lenyewe nadhani huyo Mandonga ndio kalifanya kuwa maarufu hata kabla halijafanyika. Sifuatiliagi boxing ila niliona video nyingi sana za Mandonga kabla ya pambano
 
ila jamaa katoka kinamna yake ase. Kama ilivyo kuwa kwa kanyaboya na Kilaza.
Hlf kama kapata umaarufu ghafla na amekubalika Sana Tu......binafsi namkubali Sana....

Ndo unaambiwa akikupa mungu hakuna WA kuzuia....na Kila kitu huja Kwa Wakati wake
 
Kaoneka lawama hazisaidii Bali kuna jambo la kujifunza kwa  kaka ako Mandonga, Amegeuza changamoto kuwa fursa. Kuendelea kulalama ni kutuonesha mashabiki wako hauna maturity, akili yako inafanya kazi ukiwa ulingoni lakini nje ya ulingo akili kisoda

Binafsi nilikuwa simkubali Mandonga lakini kwa sasa ni shabiki namba moja.
 
Kaoneka hapendi kujifunza kuhusu urefu wa kamba. Asiingie pango la popobawa kinyumenyume huku hana nguo hata moja mwilini.😂😂😂😂
 
Mandonga ajitahidi kidogo atakachopata akiwekeze kwenye kilimo cha matikiti

Umaarufu ni kama upepo huja na kuondooa amuulize wema sepenga ndio wa kutembeabna bodaboda kweli?
 
Back
Top Bottom