Nimekuwa mfuatiliaji wa michango ya huyu mheshimiwa shabiby kule bungeni, nimefurahishwa na namna anavyotetea rasilimali za taifa dhidi ya uhuni uliopachikwa jina la kufungua milango.
Mwanzoni nilijua huyu jamaa ni mchuuzi na mpiga deal wa mjini, aisee kumbe sikujua kuwa ni mtu makini na hazina ya taifa. Nilimsikia namna alivyochangia juu ya upandaji wa bei za mafuta kihuni huni naamini kupitia michango yake serikali iligutuka.
Juzi tena nilimsikia akielezea juu ya hii biashara kichaa ya wachina, kuwa wao wanatuzuia kwenda kwao kuna korona halafu wao wanakuja tena wanaingia kienyeji enyeji, hili liliniingia akilini na kuanza kumfuatilia huyu jamaa aisee kichawani ni mzima, halafu kuna chawa wake anaitwa msukuma, yaani anapokuwa anamwaga nondo huwa anakatizwa na chembeza za taarifa za mh musukuma.
Hongera sana shabiby nitakuja Gairo.