Shabiby; ukoo wenye 'damu ya biashara ya mabasi', satco express na shabiby line ni 'ndugu wa damu moja'

Shabiby; ukoo wenye 'damu ya biashara ya mabasi', satco express na shabiby line ni 'ndugu wa damu moja'

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Poleni na kazi wadau. Napenda kusema kwa maandishi kuwa, zipo familia hapa Tanzania zimetolewa na karama fulani. Kama ilivyokuwa kwa familia ya Rashidi Ally Matumla kuzaliwa kwa kuwa mabondia.
Kama ilivyokuwa kwa familia ya Sunday Manara kuzaliwa kwa kuwa wacheza mpira.

Kama ilivyo kwa familia ya mfanyabiashara Salimu Faraji Abri (Asasi) kuzaliwa kwa biashara ya magari makubwa (malori).

Kama ilivyo kwa familia ya Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa marais.

Ndivyo ilivyo kwa familia ya Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Mabhukut Shabiby ambaye mbali ya kuwa mwanasiasa lakini pia ni mfanyabiashara wa mabasi nchini Tanzania.

Ahmed Shabiby anamiliki mabasi ya Shabiby Line ambayo yanakwenda sehemu mbalimbali za Tanzania.
Sasa, Ahmed ana mdogo wake wa kuzaliwa, anaitwa Said Mabhukut Shabiby ambaye naye anamiliki mabasi ya kisasa yanayoitwa Satco. Satco ni kifupi cha Said Trans Company.

Familia hii, akiwemo mdogo mwingine ambaye anamiliki hoteli kubwa Dodoma ya Midland Hotel, inazidi kujipanua kwenye uwekezaji wa biashara ya mabasi ya kisasa nchini Tanzania.

Hivi karibuni, SATCO imeingiza mabasi 30 aina ya YoTong D 14 huku Shabiby Line naye akiingiza mabasi aina hiyo yenye idadi hiyo ambayo yote ni VVIP.

Satco ambaye amebeba utawala wa njia ya Dodoma-Bariadi hadi Musoma. Na pia Ratco zinafika hadi Kaskazini mwa Tanzania kwa maana ya Bukoba.

Wakati mabasi 30 ya Satco yanatoka Bandarini kwenda Dodoma, mtu mmoja mtandaoni aliandika hivi:
"Jamani jamani mliona jamani hili balaa la Satco jamani maana hili balaa sio la kusimuliwa ni la kujionea mwenyewe maana naona mwamba ameshusha Yutong D14 nyingi kama Shabiby au huyu Satco atakuwa na undugu na Shabiby maana Shabiby alishusha Yutong D14 kama utitiri naona nae Satco kaamua na yeye kujibu mapigo au hawa Satco na Shabiby watakuwa ndugu ni nini maana sio kwa kuigana huku kwa kushusha bus nyingi hivi za Yutong D14."

Ukweli ndiyo huo, Ahmed na Said Mabhukut Shabiby ni ndugu wa damu moja ambao wote 'wamejipata' kwenye biashara ya mabasi nchini Tanzania.
 

Attachments

  • FB_IMG_1750102971638.jpg
    FB_IMG_1750102971638.jpg
    202.8 KB · Views: 63
  • FB_IMG_1749987342301.jpg
    FB_IMG_1749987342301.jpg
    133 KB · Views: 55
Satco naona nae ameset standard kama za kaka yake kwa maana bus zake nae ziko na muonekano wa kuvutia sana.
 
Back
Top Bottom