Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby ameikosoa mfumo wa utoaji wa leseni kwa waendesha bodaboda, akidai kuwa gharama zinazohusiana na mafunzo na upatikanaji wa leseni ni kubwa na zinawaumiza vijana wengi wanaojishughulisha na biashara hiyo.
Akichangia mjadala wa Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27 pamoja na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27, Shabiby amesema waendesha bodaboda hulazimika kulipia mafunzo chuoni kwa ada ya takribani shilingi 100,000 kabla ya kupata leseni.
Amesema pamoja na ada hiyo, waombaji hulipa gharama nyingine ikiwemo shilingi 3,000 za mtihani wa Polisi, shilingi 10,000 za learner permit na shilingi 70,000 za leseni kutoka TRA.
“Bodaboda gani anaweza kulipa hela yote hiyo? Nani amewahi kuona bodaboda anaenda kujifunzia chuo kama sio wizi?” amehoji Shabiby.
Mbunge huyo amependekeza Polisi Kata wapewe jukumu la kutoa mafunzo na semina kwa waendesha bodaboda, kisha kuwapatia vibali vya kupata leseni badala ya kuwataka kuhudhuria mafunzo vyuoni.
Pia ameitaka TRA kupunguza gharama za leseni za bodaboda kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 50,000 ili kuwawezesha vijana wengi zaidi kuendesha shughuli zao kwa kufuata sheria.