Shabiki wa Simba apigwa mbele ya Ali Kamwe, Yanga na shabiki wachukuliwe hatua kali kwa hili

Shabiki wa Simba apigwa mbele ya Ali Kamwe, Yanga na shabiki wachukuliwe hatua kali kwa hili

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Tukio la kusikitisha limetokea baada ya mechi ya Yanga SC vs MC Alger ambapo shabiki wa Simba alipigwa na mtu wa Yanga mbele ya Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, wakati wa mahojiano na Crown Media.

Pia, Soma: FT: Yanga 0-0 MC Alger | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.01.2025

Uongozi wa Yanga unapaswa kutoa tamko kuhusu tukio hili, kwani kimya chao kinaweza kutafsiriwa kama kuunga mkono vitendo hivyo kuendelea.

Aidha, TFF inatakiwa kutoa tamko kuhusu suala hili na kuchukua hatua dhidi ya Yanga pamoja na shabiki huyo ili kukomesha vitendo visivyo vya kimpira.
 
Huyo aliepigwa unaweza kuona hana uwezo wa kuongea hivyo tofauti na mambo ya Simba na Yanga.
 
Naye kayataka,wazee wa kalkuleta wamevurgwa zao ye kawafuata!!
 
Kiherehere kimemponza,Bado Yule anaitwa Nani sijui nae manywele hiv hivi.
 
Tena yule siyo tu ni mshabiki, nadhani ni afisa kabisa wa Yanga. Sema nchi hii ndiyo hivyo kwenye ukiukwaji wa sheria tuna mambo ya "tumuachie mungu".
 
Tukio la kusikitisha limetokea baada ya mechi ya Yanga SC vs MC Alger ambapo shabiki wa Simba alipigwa na mtu wa Yanga mbele ya Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, wakati wa mahojiano na Crown Media.

Pia, Soma: FT: Yanga 0-0 MC Alger | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.01.2025

Uongozi wa Yanga unapaswa kutoa tamko kuhusu tukio hili, kwani kimya chao kinaweza kutafsiriwa kama kuunga mkono vitendo hivyo kuendelea.

Aidha, TFF inatakiwa kutoa tamko kuhusu suala hili na kuchukua hatua dhidi ya Yanga pamoja na shabiki huyo ili kukomesha vitendo visivyo vya kimpira

View attachment 3206105
Ungekua mu ungwana kipindi Cha nyuma kidogo Shabiki wa Yanga alipigwa na kuchaniwa jezi jukwaani na mashabiki wa Simba yule Big wa Simba wa Morogoro akiongoza tukio ilo pale kwa Mkapa.

Hivi si vitendo vya ki ungwana lakini tunapo kemea tusiangalie nani kufanya.
Wakati wetu sisi tulienda uwanjani pale Shamba la bibi na tulikaa kwenye mzunguko kwenye ma bomba tukiwa tumechanganyika mashabiki wa Simba na Yanga na haikuwai kuleta vurugu.

Pale Jukwaa la Pepsi Shamba la Bibi , Yanga walikaa juu Simba walikaa Chini lakini hapakuwahi kuwa na Vurugu.

Jukwaa kuu Green stand Yanga na Simba wali tenganishwa na ukuta wa chumba Cha kurushia matangazo ya redio kwa juu na eneo la wageni wa heshima , Mashabiki wa pande mbili walikua wanaweza kurushiana maneno ya utani lakini hawakua wakipigana.

Sasa iki kizazi kipya kimekuja na mambo mapya na kufikia kupigana kisa amekaa upande mwingine au ametoa maoni tofauti.
Ni ushamba wa kiwango Cha SGR.
 
Huyo shabiki ni mjinga wa kutupwa...ashukuru kwamba amepigwa kajikofi kadogo...Soka ina emotions kubwa na kali sana..hii ni duniani kote...siyo busara kukebehi wenzako kwa kipindi na wakati ule tena basi wakati mechi tu imeisha. Kwangu mimi namuona ana bahati sana. angeweza kupata madhara makubwa zaidi... hicho alichofanya ni provocation.. siku nyingine asirudie ujinga kama huo.
 
Back
Top Bottom